Local,Normal News,Singida, Azam

Ouma alia na safu ya ushambuliaji Singida BS

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Apr 2026
Ouma alia na safu ya ushambuliaji Singida BS

Kocha msaidizi wa Singida Black Stars david Ouma ameweka wazi kutoridhishwa kwake na safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kufuatia mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya hivi karibuni ya Ligi Kuu.

Akizungumza baada ya mchezo wao wa karibuni waliopoteza dhidi ya Azam Fc wakifungwa mabao 2-1 kwenye uwanja wao wa nyumbani, Ouma alisema changamoto kubwa si namna timu inavyocheza, bali ni kushindwa kutumia ipasavyo nafasi za kufunga mabao wanazozipata ndani ya dakika 90.

Alieleza kuwa kikosi chake kinauwezo wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi, lakini umakini mdogo wa washambuliaji mbele ya lango umekuwa ukiigharimu timu hiyo kupata matokeo chanya.

β€œTunacheza vizuri na tunafika mbele ya lango la wapinzani mara nyingi, lakini hatumalizii nafasi tunazozipata. Hapo ndipo tunapopoteza mechi,” alisema kocha huyo Mkenya

Katika mchezo huo, Singida Black Stars walionekana kuwa na mwanzo mzuri, lakini walishindwa kuendeleza makali yao huku Azam Fc wakitumia vyema nafasi chache walizopata kufunga mabao yaliyoamua matokeo ya mchezo.

Takwimu za Singida BS zinaonyesha kuwa imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini kiwango cha ubadilishaji wa nafasi hizo kuwa mabao kimekuwa cha chini, jambo linaloibua maswali kuhusu ufanisi wa safu ya ushambuliaji.

Baadhi ya washambuliaji waliokuwa wakitegemewa kufanya vizuri msimu huu Joseph Gueye Elvis Rupia wameonekana kupoteza makali yao, huku wengine wakishindwa kabisa kuonyesha mchango mkubwa licha ya kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kutokana na hali hiyo, Ouma amesea benchi la ufundi limeanza kutafuta suluhisho la haraka ili kuboresha safu hiyo kabla ya ratiba ngumu ya michezo ijayo, ikiwa ni pamoja na kuongeza mazoezi maalum ya kumalizia nafasi.

Kocha huyo alisisitiza kuwa bado wana imani na wachezaji waliopo, lakini ni lazima wajitathmini na kuongeza juhudi ili kurejesha ushindani wa timu hiyo katika ligi.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’