Kiungo wa Chelsea FC, Enzo Fernandez, ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo kwa michezo miwili ijayo kufuatia kauli zake alizotoa wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Kocha Liam Rosenior amethibitisha uamuzi huo, akisema mchezaji huyo hatapatikana kwa mchezo ujao pamoja na ule dhidi ya Manchester City wiki ijayo.
βKwa upande wa klabu na uamuzi wangu kama sehemu ya benchi la ufundi, hatakuwa tayari kwa mchezo wa kesho wala ule dhidi ya Manchester City. Ni jambo la kusikitisha kuzungumza kwa namna ile,β alisema Rosenior.
Kocha huyo aliongeza kuwa licha ya kumheshimu Fernandez kama mchezaji na mtu, kulikuwa na mstari ulivukwa ambao uliwalazimu kuchukua hatua za kinidhamu.
βKama tabia na utu wake sina neno baya, lakini mstari ulivukwa. Tulilazimika kuchukua hatua,β alisisitiza.
Hatua hiyo inaonesha msimamo wa Chelsea katika kudhibiti nidhamu ya wachezaji, hasa katika kipindi ambacho klabu inajaribu kurejesha utulivu na ushindani ndani ya kikosi.