International,Normal News,Chelsea

Enzo Fernandez Aachwa Kikosi cha Chelsea Baada ya Kauli Tata

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
3 Apr 2026
Enzo Fernandez Aachwa Kikosi cha Chelsea Baada ya Kauli Tata

Kiungo wa Chelsea FC, Enzo Fernandez, ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo kwa michezo miwili ijayo kufuatia kauli zake alizotoa wakati wa mapumziko ya kimataifa.

Kocha Liam Rosenior amethibitisha uamuzi huo, akisema mchezaji huyo hatapatikana kwa mchezo ujao pamoja na ule dhidi ya Manchester City wiki ijayo.

β€œKwa upande wa klabu na uamuzi wangu kama sehemu ya benchi la ufundi, hatakuwa tayari kwa mchezo wa kesho wala ule dhidi ya Manchester City. Ni jambo la kusikitisha kuzungumza kwa namna ile,” alisema Rosenior.

Kocha huyo aliongeza kuwa licha ya kumheshimu Fernandez kama mchezaji na mtu, kulikuwa na mstari ulivukwa ambao uliwalazimu kuchukua hatua za kinidhamu.

β€œKama tabia na utu wake sina neno baya, lakini mstari ulivukwa. Tulilazimika kuchukua hatua,” alisisitiza.

Hatua hiyo inaonesha msimamo wa Chelsea katika kudhibiti nidhamu ya wachezaji, hasa katika kipindi ambacho klabu inajaribu kurejesha utulivu na ushindani ndani ya kikosi.

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
6h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
8h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
8h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’