Local,Normal News,Dodoma, Fountain, KMC, Mbeya

Dodoma Jiji, Mbeya City zatakata ligi kuu, Fountain, KMC mambo magumu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Apr 2026
Dodoma Jiji, Mbeya City zatakata ligi kuu, Fountain, KMC mambo magumu

Timu ya Dodoma Jiji imepanda hadi nafasi ya saba katika msimamo wa NBC Premier League baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo uliochezwa Ijumaa uwanja wa Airtel, Singoda.

Katika mchezo huo uliotawaliwa na Dodoma Jiji, Augustino Nsata aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya 36, ikifuatiwa na Idd Kipagwile kuongeza la pili dakika ya 69. Kassim Mgaza alihitimisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya nyongeza 90+2, akihakikishia timu yake pointi tatu muhimu.

Ushindi huo umeifanya Dodoma Jiji kufikisha alama 24 na kupanda hadi nafasi ya saba, hatua inayowaweka kwenye eneo salama la msimamo wa ligi, huku Fountain Gate wakishuka hadi nafasi ya 13 na presha ya kushuka daraja ikianza kuonekana wazi.

Katika pambano lingine lililosisimua, Mbeya City iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya KMC. Riphat Msuya alifunga bao la kwanza dakika ya 65, akifuatwa na Adilly Buha kufunga penalti dakika ya 77, huku Said Naushad akimalizia ushindi kwa kufunga bao la tatu dakika ya 87.

KMC walijibu kwa mabao ya Paul Adam dakika ya 45 na Adam Uledi dakika ya 79, lakini hawakuweza kuudhibiti ushindi wa Mbeya City. Ushindi huu umewasogeza Mbeya City hadi nafasi ya 12 na kufikisha alama 16, wakati KMC wanaendelea kuburuza mkia wa ligi, jambo linaloongeza presha kubwa ya kupambana na hatari ya kushuka daraja.

Matokeo ya michezo hiyo miwili yamezidi kuongeza ushindani katika ligi hiyo, hususan kwa timu zilizopo katikati ya jedwali pamoja na zile zinazopambana kujinusuru kushuka daraja.Β 

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
6h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
10h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
16h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
16h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
22h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’