Klabu ya KMC imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Abdallah Mohamed 'Bares' kufuatia kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu jana.
Bares alitua KMC kuchukua nafasi ya Marcio Maximo hata hivyo nae ameshindwa kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo.
KMC wanaendelea kuburuza mkia katika msimamo wa ligi wakiwa na alama nane tu. Wako katika hatari kubwa ya kushuka daraja.




