Local,Normal News,Simba, Yanga

Rage aishauri Simba iachane na shauri la Damaro

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Apr 2026
Rage aishauri Simba iachane na shauri la Damaro

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba SC, Ismail Aden Rage, ameishauri klabu hiyo kuachana na sakata la kiungo wa Yanga, Mohamed Damaro Camara, akisema kuendelea kulifuatilia ni kupoteza muda na nguvu bila sababu ya msingi.

Rage alitoa kauli hiyo yakiwa ni maoni yake akisisitiza kuwa hakuna faida kwa Simba kuendelea kushinikiza suala hilo baada ya uamuzi uliotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulimaliza.

β€œMimi nawashauri viongozi wangu waachane na jambo hili, linatupotezea muda tu, hata tukienda CAS hatuwezi kushinda hivyo ni bora tukijikite kwenye mambo ya msingi yenye manufaa kwa klabu yetu,” alinukuliwa Rage akieleza.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya TFF, kupitia kamati yake husika, kutoa uamuzi wa kutupilia mbali malalamiko ya Simba yaliyokuwa yanahoji uhalali wa usajili wa Damaro.

Katika uamuzi huo uliotolewa Aprili 2, 2026, TFF ilieleza kuwa hakukuwa na ukiukwaji wowote wa kanuni za usajili, hivyo kumruhusu mchezaji huyo kuendelea kuitumikia Yanga bila kikwazo.

Awali, Simba walikuwa wamewasilisha malalamiko wakidai kuwa Yanga walikiuka kanuni kwa kuzidisha idadi ya wachezaji wa kigeni, hoja ambayo ilipingwa na kutupiliwa mbali baada ya uchunguzi.

Pamoja na uamuzi huo, taarifa zinaeleza kuwa Simba walikuwa wakifikiria kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), hatua ambayo Rage ameionya kuwa inaweza isibadili uamuzi wa TFF zaidi ni kupoteza muda na fedha.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’