Local,Normal News,Azam, Simba

Ili tushinde ni lazima tuwe bora kuliko Simba - Ibenge

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Apr 2026
Ili tushinde ni lazima tuwe bora kuliko Simba - Ibenge

Kocha Mkuu wa Azam Fc Florent Ibenge amesema mechi ya ligi kuu dhidi ya Simba itakayopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Azam Complex, inazikutanisha timu bora ambazo ziliiwakilisha Tanzania katika michuano ya CAF msimu huu.

Ibenge amesema ili kuweza kushinda mchezo huo watalazimika kupandisha kiwango chao na kuwazidi Simba.

"Simba Sc sio timu ndogo, ni miongoni mwa timu bora kabisa hapa Tanzania, ukiangalia vile wanavyocheza ni wazi utaona wanacheza vizuri"

"Ni timu nzuri, hivyo mechi dhidi ya Simba sio sawa na mechi unazocheza dhidi ya timu nyingine"

"Walikuwa hatua ya makundi ligi ya mabingwa (CAFCL) sisi tulikuwa kombe la Shirikisho (CAFCC) hivyo tunakwenda kucheza mechi kubwa itakayokutanisha timu zilizocheza makundi CAF"

"Kucheza mechi za aina hii ni lazima tupandishe kiwango chetu hivyo tutapaswa kuwa bora dhidi ya Simba ili tuweze kuibuka na ushindi," alisema Ibenge

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’