Yanga yajiimarisha kileleni ligi kuu, yaichapa Prisons 3-0

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Apr 2026
Yanga yajiimarisha kileleni ligi kuu, yaichapa Prisons 3-0

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wamejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha alama 41, huku ukiwa ni muhimu baada ya kukaa kwa dakika 270 bila kupata ushindi.

Katika mchezo huo, Yanga ilianza kwa kasi na kutawala kwa kiasi kikubwa kipindi cha kwanza, lakini safu ya ulinzi ya Tanzania Prisons ilionyesha uimara na kufanikiwa kuhimili mashambulizi ya wapinzani wao hadi mapumziko yalipofika huku matokeo yakiwa 0-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko ya kimkakati kutoka kwa Yanga, wakianza kutumia zaidi mashambulizi ya pembeni hali iliyowazaa matunda mapema.

Dakika ya 50, kiungo mshambuliaji Allan Okello aliipatia Yanga bao la kuongoza akimalizia krosi ya Israel Mwenda.

Bao hilo lilifungua mchezo zaidi huku Tanzania Prisons wakilazimika kusogea mbele kutafuta bao la kusawazisha, lakini hali hiyo iliwaacha wazi nyuma.

Dakika ya 68, Mudathir Yahya aliongeza bao la pili akimalizia pasi safi kutoka kwa Okello, akiendeleza presha kwa wapinzani wao.

Yanga iliendelea kutawala mchezo huo na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 86 kupitia Pacome Zouzoua, aliyemzunguka kipa wa Prisons, Moussa Mbissa, baada ya kupokea pasi mpenyezo kutoka kwa Duke Abuya.

Awali, Zouzoua alifunga bao lililokataliwa kwa madai ya kuotea, lakini hakukata tamaa na kufanikiwa kufunga bao halali lililohitimisha ushindi huo.

Kwa matokeo hayo, Yanga inaendelea kuonyesha dhamira ya kutetea ubingwa wake, huku Tanzania Prisons ikiendelea kusalia kwenye wakati mgumu katika msimamo wa ligi.

Ushindi huo pia unaongeza morali kwa kikosi cha Yanga kuelekea michezo ijayo ya ligi.

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
50m ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
2h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
3h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
7h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
9h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
10h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’