Klabu ya Southampton inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) imeandika historia baada ya kuiondoa Arsenal FC katika hatua ya robo fainali ya FA Cup.
Katika mchezo huo uliowashtua wengi, Southampton walionyesha kiwango cha juu na kufanikiwa kupata ushindi muhimu uliowavusha mpaka hatua ya nusu fainali huku mabao yakifungwa na nyota wao Ross Stewart (29) na Shea Charles (22) huku bao pekee la Arsenal likifungwa na mshambuliaji wao Victor Gyökores.
Kwa upande wa Arsenal, huu unakuwa ni muendelezo wa matokeo mabaya baada ya kupokea kipigo cha pili mfululizo, hali inayozidi kuongeza presha kwa kocha Mikel Arteta.
Kuondolewa huko kunamaanisha kuwa Arsenal wamepoteza nafasi ya kushinda makombe yote ya ndani (domestic cups), na sasa matumaini yao ya taji yamebaki katika Premier League na UEFA Champions League pekee.
Matokeo hayo pia yamezua mjadala mkubwa miongoni mwa wachambuzi na mashabiki kuhusu mustakabali wa Arteta, huku swali likiwa kama atahesabika kufeli iwapo atamaliza msimu bila taji tena.