PSV Watwaa Ubingwa wa Eredivisie kwa Mara ya 27 Mfululizo wa Tatu

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 5th April 2026


PSV Watwaa Ubingwa wa Eredivisie kwa Mara ya 27 Mfululizo wa Tatu

Klabu ya PSV Eindhoven imetangazwa rasmi kuwa mabingwa wa Eredivisie baada ya wapinzani wao wakuu Feyenoord kutoka sare katika mchezo wao wa leo dhidi ya Fc Volendam.

Huu ni ubingwa wa 27 kwa PSV katika historia ya klabu hiyo, na wa tatu mfululizo, hatua inayothibitisha ubora wao na uthabiti mkubwa ndani ya soka la Uholanzi.

PSV wameendelea kutawala ligi hiyo kwa kiwango cha juu, wakionesha ushindani mkali na kuacha pengo dhidi ya wapinzani wao katika msimamo wa ligi.

Ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo, yakionyesha enzi mpya ya ubabe wao ndani ya Eredivisie.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.