Local,Normal News,Azam, Simba

Azam Fc, Simba hakuna mbabe

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Apr 2026
Azam Fc, Simba hakuna mbabe

Timu za Azam FC na Simba SC zimetoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Jumapili, Aprili 5, 2026, kwenye Uwanja wa Azam Complex Stadium

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulizikutanisha timu hizo mbili zinazowania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi, huku kila upande ukionyesha umakini mkubwa hasa katika safu ya ulinzi.

Walinda lango Aishi Manula wa Azam FC na Djibrill Kassali wa Simba kw nyakati tofauti walilazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa hatari langoni. Makipa hao walifanya mfululizo wa uokoaji na kuzuia mashuti ya hatari yaliyolenga nyavu zao.

Katika eneo la kiungo, kulishuhudiwa mapambano makali ya kumiliki mpira ambapo Azam FC walimtegemea James Akaminko, Himid Mao na Feisal Salum, huku Simba SC wakijibu mapigo kupitia Yusuph Kagoma, Allasane Kante pamoja na Clatous Chama.

Katika kipindi cha pili, Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa Chama na nafasi yake kuchukuliwa na Neo Maema, hatua iliyolenga kuongeza nguvu ya ushambuliaji, lakini haikuzaa matunda yaliyotarajiwa.

Licha ya kumalizika kwa sare ya bila mabao, mchezo huo ulikuwa wa wazi na wenye kasi, huku kila timu ikitengeneza nafasi kadhaa za kufunga. Hata hivyo, ukosefu wa umakini katika umaliziaji wa nafasi hizo uliwanyima mashabiki fursa ya kushuhudia mabao.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’