International,Normal News,Local, Barcelona, Real Madrid

Vini Jr ampa moyo Lamine baada ya kubaguliwa

Joel JJ By Joel JJ
6 Apr 2026
Vini Jr ampa moyo Lamine baada ya kubaguliwa

Katika ujumbe wa umoja na kukemea ubaguzi, Vinícius Júnior, kiungo mshambuliaji mahiri wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil, ameonyesha sapoti yake kwa Lamine Yamal, nyota kijana wa FC Barcelona, kufuatia matukio ya kauli za ubaguzi zilizosikika uwanjani hivi karibuni.

Hii imejiri baada ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Hispania na Misri uliochezwa RCDE Stadium mjini Barcelona, ambapo baadhi ya mashabiki waliibua kauli chafu za kinidhamu zinazohusiana na ubaguzi wa kiislamu.

Tukio hilo limesababisha polisi wa Hispania kuanzisha uchunguzi kuhusu chanzo na athari za kauli hizo zenye asili ya ubaguzi wa kikabila na kidini.

Katika hali iliyozua mjadala mkubwa, Yamal, ambaye ni Muislamu, alichukua nafasi kwenye mtandao wa kijamii kueleza hisia zake kuhusu kauli hizo, akisema zilikuwa “haina heshima na zisizovumilika,” licha ya kutambua kuwa zilikuwa zikielekezwa kwa wapinzani wao wa uwanjani na si yeye binafsi.

Katika ujumbe wake wa kuonyeshamshikamano, Vinícius Jr aliendelea kuonyesha msaada kwa kijana huyo wa Barcelona, akizungumza kuhusu umuhimu wa vita dhidi ya ubaguzi unaoendelea kuibuka katika soka la Ulaya.

Kiungo huyo mshambuliaji, ambaye yeye mwenyewe amekuwa akipigwa vita na kauli chafu za ubaguzi nchini Hispania katika miaka ya hivi karibuni, aliitaka jamii ya wachezaji kuungana dhidi ya vitendo vya ubaguzi na kushirikiana kupambana navyo.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE →