Local,Normal News,TRA, Simba

TRA United vs Simba; Tiketi za mechi ya awali kutumika

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Apr 2026
TRA United vs Simba; Tiketi za mechi ya awali kutumika

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeutaarifu umma kuwa mchezo namba saba (7) wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026 (TRA United FC vs Simba SC), utafanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Aprili 9, 2026 kuanzia saa 10:00 alasiri.

Aidha, Bodi imetoa taarifa kuwa mashabiki wote ambao walinunua tiketi kwa ajili ya mchezo huo ambao uliahirishwa Machi 14, 2026 baada ya mvua kubwa kunyesha jijini Arusha na kusababisha uwanja kukosa sifa za kisheria, watatumia tiketi hizo kuingia uwanjani katika mchezo wa Aprili 9, 2026, ambapo shabiki atalazimika kuwa na kadi (N-CARD) ambayo aliitumia kununua tiketi ya mchezo ulioahirishwa, kwa ajili ya uhakiki getini.

Tayari wauzaji wa tiketi za mchezo huo, National Internet Data Center (NIDC) wamerejesha tiketi zote zilizonunuliwa, kwenye kadi za mashabiki hao bila kujali shabiki alikuwa ameshaingia uwanjani ama hakuingia kabisa, na kwamba mashabiki hao hawatapaswa kununua tena tiketi. Tiketi ambazo ziliuzwa katika mchezo huo ni VVIP 95, VIP 567 na Mzunguko 3,215.

Bodi inawakumbusha mashabiki ambao hawakununua tiketi kwenye mchezo ulioahirishwa, kuwa tiketi zinapatikana (zinauzwa) kwenye vituo vya N-CARD vya kuuzia tiketi na kupitia mitandao ya simu kwa gharama zifuatazo;

  • VVIP – 50,000

  • VIP (Wing A & B) – 30,000

  • Mzunguko – 10,000

Bodi ya Ligi inawashukuru sana mashabiki wa mpira wa miguu kwa ushirikiano mkubwa wanaozidi kuutoa kwa Bodi na klabu zake, ikiwemo kununua tiketi na kuingia viwanjani kuziuunga mkono klabu zetu.

Imetolewa na;
Idara ya Habari na Mawasiliano Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Aprili 8, 2026

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
43m ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
4h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
5h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
7h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
7h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
11h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
13h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
14h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’