Local,Normal News,Yanga, TMA

TMA Stars kuivurugia Yanga rekodi leo?

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Apr 2026
TMA Stars kuivurugia Yanga rekodi leo?

Leo mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la CRDB Yanga watashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili TMA Stars katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo. Mtanange huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 kwa saa za Afrika Mashariki.

Yanga itaingia kwenye mchezo huku ikiwa na rekodi ya aina yake katika michuano hiyo inayodhaminiwa na benki ya CRDB.

Mara ya mwisho Yanga kupoteza mchezo wa Kombe la Shirikisho nchini Tanzania ilikuwa Julai 26,2021 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba uliochezwa dimba la Lake Tanganyika Mkoani Kigoma ambapo Simba waliifunga Yanga bao 1-0 lililofungwa na Taddeo Lwanga dakika ya 79' ya mchezo na kuipa Simba ubingwa.

Tangu mchezo huo mpaka sasa Yanga haijawahi kupoteza mchezo wowote ule kwenye michuano hiyo. zikiwa zimepita siku 1,721 awa na wiki 245 na siku 6.

Ni sawa na miaka 4, miezi 8 na siku 17 ambayo pia ni sawa na masaa 41,304. Leo Wananchi watakuwa wakiisaka tiketi ya robo fainali mbele ya TMA Stars ambayo yawezekana ikaonekana ni timu nyepesi lakini hawajafika hatua ya 16 bora kwa bahati mbaya.Β 

Je Wananchi wataendeleza ubabe wao katika michuano hiyo au ule msemo wa 'mende kudondosha kabati' unaweza kutimia?

More Stories

Nyota Geita Gold afunguka rafu ya Aziz KI, Ilikuwa bahati mbaya
Nyota Geita Gold afunguka rafu ya Aziz KI, Ilikuwa bahati mbaya
2h ago
READ MORE β†’
LAPORTA: Atletico kumuuza Alvarez kwa timu yeyote isipokuwa Barcelona
LAPORTA: Atletico kumuuza Alvarez kwa timu yeyote isipokuwa Barcelona
4h ago
READ MORE β†’
Ngorongoro Heroes yatangulia nusu fainali CECAFA U20 kwa kishindo
Ngorongoro Heroes yatangulia nusu fainali CECAFA U20 kwa kishindo
6h ago
READ MORE β†’
Samatta afunga bao lake la pili, Le Havre ikipoteza
Samatta afunga bao lake la pili, Le Havre ikipoteza
6h ago
READ MORE β†’
Salah hakamatiki Uturuki, apiga hat-trik Trabzonspor ikiifumua Galatasaray 4-0
Salah hakamatiki Uturuki, apiga hat-trik Trabzonspor ikiifumua Galatasaray 4-0
7h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaonywa, Yanga yakumbana na faini - Kamati ya saa 72
Azam Fc yaonywa, Yanga yakumbana na faini - Kamati ya saa 72
7h ago
READ MORE β†’
Mshambuliaji wa zamani Yanga aibukia Zambia
Mshambuliaji wa zamani Yanga aibukia Zambia
7h ago
READ MORE β†’
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
15h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
19h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
20h ago
READ MORE β†’