Leo mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la CRDB Yanga watashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili TMA Stars katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo. Mtanange huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
Yanga itaingia kwenye mchezo huku ikiwa na rekodi ya aina yake katika michuano hiyo inayodhaminiwa na benki ya CRDB.





