Local,Normal News,Simba, Fountain, Coastal, Dodoma

Fountain Gate mikononi mwa Mnyama mkali Arusha leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Apr 2026
Fountain Gate mikononi mwa Mnyama mkali Arusha leo

Mikiki mikiki ya Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo huku mashabiki wa soka nchini wakishuhudia michezo miwili muhimu itakayopigwa katika viwanja tofauti. Macho mengi yataelekezwa mkoani Arusha, wakati mchezo mwingine ukipigwa jijini Tanga.

Katika dimba la Sheikh Amri Abeid, Fountain Gate FC watakuwa wenyeji wa Simba SC kwenye mchezo wa kiporo wa mzunguko wa 17. Huu ni mchezo unaobeba uzito mkubwa kwa Simba katika mbio za ubingwa msimu huu.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kucheza mara mbili tayari kwenye uwanja huo ndani ya wiki moja, ikiwemo dhidi ya TRA United pamoja na Dodoma Jiji FC katika michuano ya Kombe la CRDB. Uzoefu huo unaweza kuwa faida kwa Wekundu wa Msimbazi wanapotafuta ushindi muhimu leo.

Kwa upande wa msimamo wa ligi, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 36, ikiwafukuzia Young Africans SC waliopo kileleni na alama 44, huku Yanga ikiwa imecheza mechi moja zaidi. Hivyo basi, hakuna matokeo mengine yanayokubalika kwa Simba zaidi ya ushindi ili kupunguza pengo la pointi na kuendelea kuweka hai matumaini ya ubingwa.

Simba itaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na mapungufu kidogo kikosini, baada ya kukosa huduma ya nyota wake wawili muhimu, Shomari Kapombe na Yusuph Kagoma ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kwa upande wa wenyeji Fountain Gate, wanaingia uwanjani wakijaribu kupambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja. Timu hiyo inayoshika nafasi ya 14 imekuwa ikifanya mabadiliko ya kiufundi, ikiwemo kumteua Fredy Felix Minziro kuwa kocha mkuu hivi karibuni. Hata hivyo, wanakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya Simba, na huenda wakalenga angalau kupata alama moja.

Wakati huo huo, katika dimba la Mkwakwani jijini Tanga, Coastal Union FC watakuwa nyumbani kuikaribisha Dodoma Jiji FC katika mchezo mwingine wa ligi. Huu pia ni mchezo muhimu kwa timu zote mbili katika kuhakikisha zinajiweka salama kwenye msimamo wa ligi.

More Stories

Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
4h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
4h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
7h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
10h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
12h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
13h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’
Kocha Dimitar Pantev ateuliwa kuwa kocha mpya wa Richard Bay.
Kocha Dimitar Pantev ateuliwa kuwa kocha mpya wa Richard Bay.
1d ago
READ MORE β†’