International,Normal News,Arsenal, Manchester City

Arteta azua gumzo ndani ya Arsenal

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
17 Apr 2026
Arteta azua gumzo ndani ya Arsenal

Kocha wa Arsenal FC, Mikel Arteta, ameibua mjadala mkubwa baada ya kufichuliwa kwa mbinu zake zisizo za kawaida za kuwaandaa wachezaji wake kisaikolojia kabla ya mechi muhimu.

Kwa mujibu wa ripoti ya The Athletic, Arteta aliwahi kuwasha moto halisi katika uwanja wa mazoezi wa London Colney kama sehemu ya kuwajengea wachezaji wake hisia ya β€œkuwa moto” kabla ya pambano lao dhidi ya Sporting CP katika UEFA Champions League.

Inaelezwa kuwa kabla ya mechi hiyo, Arteta alizungumza na wachezaji wake kuhusu umuhimu wa kuingia uwanjani wakiwa na ari ya hali ya juu, lakini badala ya kubaki kwenye maneno tu, aliamua kuonesha hali hiyo kwa vitendo, hatua iliyowashangaza wengi ndani ya kikosi.

Hii si mara ya kwanza kwa Arteta kutumia mbinu za kipekee za kisaikolojia. Awali aliwahi kutumia vielelezo vya picha za wanyama kama mbwa mwitu ili kuhamasisha umoja na ari ya ushindani ndani ya timu. Mbinu hizo zina lengo la kuwafanya wachezaji β€œkuhisi” zaidi kuliko kusikia tu maelekezo ya kawaida ya kiufundi.

Wapo wanaoona hatua hizo kama ubunifu unaochangia mafanikio ya timu, hasa ikizingatiwa kuwa Arsenal wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Champions League. Hata hivyo, wengine wanaibua maswali kuhusu usalama na ufanisi wa mbinu hizo kwa kila mchezaji.

Licha ya mjadala huo, matokeo ya uwanjani yanaonekana kuipa nguvu falsafa ya Arteta, ambaye anaamini kuwa mafanikio ya soka hayaanzi tu kwa mbinu za kiufundi bali pia katika maandalizi ya kisaikolojia ya wachezaji.

Kwa sasa, Arsenal wanaendelea na safari yao ya Ulaya wakiwa na matumaini makubwa, huku mbinu za Arteta zikiendelea kuwa sehemu ya mjadala mkubwa ndani na nje ya uwanja, hususani katika mechi inayowakabili mbeleni dhidi ya Manchester City.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
6h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
10h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
11h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
13h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
13h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
17h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
19h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
19h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’