Manchester United yaamua, Bruno Fernandes hauzwi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th April 2026

Manchester United yaamua, Bruno Fernandes hauzwi

Kiungo nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, amepewa uhakika wa mustakabali wake klabuni hapo kufuatia taarifa mpya zinazoonyesha kuwa hataruhusiwa kuondoka katika dirisha lijalo la usajili.

Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, uongozi wa Manchester United umeweka wazi kuwa hauna mpango wowote wa kumuachia nyota huyo, ukisisitiza kuwa hatouzwa β€œkwa hali yoyote” katika majira ya joto yajayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya kipindi cha sintofahamu kilichohusisha ofa kubwa kutoka klabu za Saudi Arabia, ikiwemo ofa ya Al-Nassr iliyodaiwa kufikia pauni milioni 80. Hata hivyo, mabosi wa United sasa wamebadilisha msimamo na kumhakikishia nahodha wao kuwa ni sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya klabu.Β 

Ripoti nyingine zinaeleza kuwa klabu pia imeanza juhudi za kuharakisha mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ili kumfunga zaidi kiungo huyo, ambaye tayari ana mkataba unaoelekea kumalizika ndani ya kipindi kifupi kijacho.Β 

Mbali na msimamo huo wa klabu, Fernandes mwenyewe ameonyesha dalili za kuridhika kuendelea kubaki Old Trafford, akisisitiza furaha yake na nafasi yake ndani ya timu hiyo.Β 

Kwa sasa, nyota huyo anaendelea kuwa mhimili muhimu wa kikosi cha United, akichangia mabao na pasi za mwisho huku akiongoza timu kama nahodha. Uongozi wa klabu unaamini kuwa mafanikio ya msimu huu, ikiwa ni pamoja na mbio za kufuzu michuano ya Ulaya, yatasaidia zaidi kumshawishi kubaki.

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE β†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE β†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE β†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE β†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE β†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE β†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE β†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE β†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE β†’