Chelsea waendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya, Manguli watajwa kurithi mikoba

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media โ€ข 24th April 2026


Chelsea waendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya, Manguli watajwa kurithi mikoba

Klabu ya Chelsea imeanza rasmi mchakato wa kutafuta kocha mpya kuelekea msimu ujao, huku majina kadhaa makubwa yakitajwa kuwania nafasi hiyo muhimu ndani ya Stamford Bridge, kama ilivyoripotiwa na Fabrizio Romano.

Hatua hiyo inakuja wakati klabu hiyo ikipitia kipindi kigumu cha matokeo na mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi, hali inayolazimisha uongozi kutafuta suluhisho la kudumu.

Miongoni mwa makocha wanaotajwa kupewa nafasi kubwa ni Andoni Iraola, ambaye ameonyesha mafanikio makubwa akiwa na AFC Bournemouth. Iraola anasifiwa kwa mtindo wake wa kisasa wa soka unaochanganya nguvu, kasi na mbinu, pamoja na uzoefu wake ndani ya Premier League.

Pia anatajwa Filipe Luรญs, ambaye kwa sasa anaongoza CR Flamengo kwa mafanikio. Akiwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, anaifahamu vyema klabu hiyo, ingawa uzoefu wake kama kocha barani Ulaya bado ni mdogo.

Chaguo jingine ni Frank Lampard, legenda wa klabu hiyo ambaye tayari aliwahi kuinoa timu hiyo hapo awali. Lampard anaungwa mkono na sehemu ya mashabiki, lakini kumbukumbu ya matokeo yake ya mwisho akiwa kocha bado inaibua maswali.

Aidha, jina la Cesc Fร bregas pia linatajwa, kufuatia kazi yake nzuri akiwa na Como 1907 nchini Italia. Hata hivyo, uzoefu wake mdogo katika miradi mikubwa unatajwa kuwa changamoto inayoweza kuathiri nafasi yake.

Majina mengine yanayotajwa kuhusishwa kurithi mikoba ya Rosenior ni kama, Marco Silver (Fulham), Xabi alonso na Luis Enrique (PSG).

Chelsea wanaripotiwa kupanga kufanya mabadiliko makubwa majira ya joto, ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wenye uzoefu zaidi ili kuleta uwiano ndani ya kikosi, pamoja na kumpa kocha mpya nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya usajili.

Tangu mwaka 2021, klabu hiyo imebadilisha makocha mara kadhaa, hali inayochochea hitaji la kupata suluhisho la muda mrefu litakalorejesha utulivu na ushindani ndani ya timu.

Kwa sasa, macho yote yanaelekezwa Stamford Bridge huku wadau wakisubiri kuona nani atapewa jukumu la kuiongoza Chelsea katika sura mpya ya klabu hiyo.


  

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE โ†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE โ†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE โ†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE โ†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE โ†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE โ†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE โ†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE โ†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE โ†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE โ†’