Chelsea waendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya, Manguli watajwa kurithi mikoba

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
•
24 Apr 2026
Chelsea waendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya, Manguli watajwa kurithi mikoba

Klabu ya Chelsea imeanza rasmi mchakato wa kutafuta kocha mpya kuelekea msimu ujao, huku majina kadhaa makubwa yakitajwa kuwania nafasi hiyo muhimu ndani ya Stamford Bridge, kama ilivyoripotiwa na Fabrizio Romano.

Hatua hiyo inakuja wakati klabu hiyo ikipitia kipindi kigumu cha matokeo na mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi, hali inayolazimisha uongozi kutafuta suluhisho la kudumu.

Miongoni mwa makocha wanaotajwa kupewa nafasi kubwa ni Andoni Iraola, ambaye ameonyesha mafanikio makubwa akiwa na AFC Bournemouth. Iraola anasifiwa kwa mtindo wake wa kisasa wa soka unaochanganya nguvu, kasi na mbinu, pamoja na uzoefu wake ndani ya Premier League.

Pia anatajwa Filipe Luís, ambaye kwa sasa anaongoza CR Flamengo kwa mafanikio. Akiwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, anaifahamu vyema klabu hiyo, ingawa uzoefu wake kama kocha barani Ulaya bado ni mdogo.

Chaguo jingine ni Frank Lampard, legenda wa klabu hiyo ambaye tayari aliwahi kuinoa timu hiyo hapo awali. Lampard anaungwa mkono na sehemu ya mashabiki, lakini kumbukumbu ya matokeo yake ya mwisho akiwa kocha bado inaibua maswali.

Aidha, jina la Cesc Fàbregas pia linatajwa, kufuatia kazi yake nzuri akiwa na Como 1907 nchini Italia. Hata hivyo, uzoefu wake mdogo katika miradi mikubwa unatajwa kuwa changamoto inayoweza kuathiri nafasi yake.

Majina mengine yanayotajwa kuhusishwa kurithi mikoba ya Rosenior ni kama, Marco Silver (Fulham), Xabi alonso na Luis Enrique (PSG).

Chelsea wanaripotiwa kupanga kufanya mabadiliko makubwa majira ya joto, ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wenye uzoefu zaidi ili kuleta uwiano ndani ya kikosi, pamoja na kumpa kocha mpya nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya usajili.

Tangu mwaka 2021, klabu hiyo imebadilisha makocha mara kadhaa, hali inayochochea hitaji la kupata suluhisho la muda mrefu litakalorejesha utulivu na ushindani ndani ya timu.

Kwa sasa, macho yote yanaelekezwa Stamford Bridge huku wadau wakisubiri kuona nani atapewa jukumu la kuiongoza Chelsea katika sura mpya ya klabu hiyo.

ADVERTISE HERE

More Stories

Raphinha aongeza mkataba Barcelona hadi 2030
Raphinha aongeza mkataba Barcelona hadi 2030
47m ago
READ MORE →
Yanga yakaribia kumnasa Fadlu Davids kuwa kocha Mkuu
Yanga yakaribia kumnasa Fadlu Davids kuwa kocha Mkuu
1h ago
READ MORE →
Cristiano Ronaldo atangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa
Cristiano Ronaldo atangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa
3h ago
READ MORE →
Carragher aibua maswali kuhusu usajili wa Liverpool
Carragher aibua maswali kuhusu usajili wa Liverpool
3h ago
READ MORE →
Singida Black Stars yazidi kubomoka, Chasambi naye avunja mkataba
Singida Black Stars yazidi kubomoka, Chasambi naye avunja mkataba
3h ago
READ MORE →
Mpanzu, Barker watwaa tuzo za Ligi Kuu Oktoba 2026
Mpanzu, Barker watwaa tuzo za Ligi Kuu Oktoba 2026
6h ago
READ MORE →
Waamuzi wa Tanzania wateuliwa kusimamia mchezo wa kufuzu AFCON 2027
Waamuzi wa Tanzania wateuliwa kusimamia mchezo wa kufuzu AFCON 2027
7h ago
READ MORE →
Liverpool aangukia pua Uturuki, Real Madrid yaibuka na ushindi wa dakika za mwisho
Liverpool aangukia pua Uturuki, Real Madrid yaibuka na ushindi wa dakika za mwisho
16h ago
READ MORE →
Haina kupoa! UEFA Champions League kuendelea leo kwa michezo ya kibabe
Haina kupoa! UEFA Champions League kuendelea leo kwa michezo ya kibabe
1d ago
READ MORE →
Dosari za mabilioni zaibuka ukarabati wa viwanja vya Afcon 2027
Dosari za mabilioni zaibuka ukarabati wa viwanja vya Afcon 2027
1d ago
READ MORE →