International,Normal News,Bayern, Mainz

Bayern mabingwa, waendeleza wimbi la ushindi Bundesliga

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Apr 2026
Bayern mabingwa, waendeleza wimbi la ushindi Bundesliga

Klabu ya Bayern Munich imeendelea kuonyesha ubabe wake katika Bundesliga baada ya kuibuka na ushindi wa kusisimua wa mabao 4-3 dhidi ya Mainz 05 katika mchezo uliochezwa Jumamosi, Aprili 25, 2026.

Katika mchezo huo wa kusisimua uliopigwa kwenye dimba la MEWA Arena, Bayern walijikuta wakicheza chini ya kiwango kipindi cha kwanza baada ya kuruhusu mabao matatu kutoka kwa Mainz, yaliyofungwa na Dominik Kohr, Paul Nebel na Sheraldo Becker.Β 

Hata hivyo, mabingwa hao tayari wa Bundesliga walirudi kwa nguvu kipindi cha pili na kuonyesha kwa nini wanaitwa mabingwa. Nicolas Jackson alianza kurejesha matumaini kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 53 kabla ya Michael Olise kupunguza pengo zaidi dakika ya 73.

Shinikizo liliendelea kuongezeka kwa Mainz baada ya Jamal Musiala kusawazisha dakika ya 80, kabla ya mshambuliaji hatari Harry Kane kufunga bao la ushindi dakika ya 83 na kukamilisha comeback ya ajabu.

Ushindi huo unaifanya Bayern kuendeleza rekodi yao nzuri ya ushindi mfululizo, ikiwa ni moja ya dalili za uimara mkubwa waliouonyesha msimu huu.Β 

Bayern tayari walikuwa wametangazwa mabingwa wa Bundesliga kabla ya mchezo huo, baada ya ushindi wao dhidi ya Stuttgart uliowahakikishia taji la msimu wa 2025/26.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
8h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
10h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
12h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
14h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
15h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
20h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’