Mashujaa yaiduwaza TRA United wakati Mbeya City ikishinda Mbeya Derby

Joel JJ By Joel JJ β€’ 4th May 2026

Mashujaa yaiduwaza TRA United wakati Mbeya City ikishinda Mbeya Derby

Ligi Kuu NBC imeendelea leo kwa michezo miwili kupigw katika miji ya Kigoma na Mbeya.

Mashujaa FC waibuka na ushindi Kigoma

Katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, Mashujaa FC waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya TRA United.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na Ismail Mgunda dakika ya 37, bao lililodumu hadi mwisho wa dakika 90. Ushindi huo unaipa Mashujaa alama muhimu katika harakati zao za kupanda juu ya msimamo wa ligi.

TRA United walijaribu kusawazisha katika kipindi cha pili lakini walishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Mashujaa iliyokuwa imara.

Mbeya Derby: Mbeya City yaibuka kidedea

Katika dabi ya jiji la Mbeya, uwanja wa Sokoine, Mbeya City waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliokuwa na presha kubwa kwa pande zote.

Mbeya City walianza vyema kwa kupata bao la kuongoza kupitia Eliud Ambokile dakika ya 19. Hata hivyo, Tanzania Prisons walirejea mchezoni baada ya Emmanuel Martin kusawazisha dakika ya 33.

Katika kipindi cha pili, presha ya Mbeya City ilizaa matunda baada ya beki wa Prisons, Martin Mhilu, kujifunga na kuipa Mbeya City bao la ushindi.

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE β†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE β†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE β†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE β†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE β†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE β†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE β†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE β†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE β†’