Yanga yakumbana na rungu la Kamati ya saa 72

Joel JJ By Joel JJ β€’ 11th May 2026

Yanga yakumbana na rungu la Kamati ya saa 72

Maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kufuatia kikao cha tarehe 9 Mei, 2026:

1. Ligi Kuu ya NBC

Mechi: Simba SC 2-2 Young Africans (Mechi Na. 169)

Kamati imetoa adhabu kadhaa kwa klabu ya Yanga kufuatia mchezo huu uliopigwa Mei 3, 2026:

  • Kuchelewa kufika uwanjani: Klabu imepewa Onyo Kali kwa kufika uwanjani saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri.

  • Kususia chumba cha kuvalia: Klabu imetozwa faini ya Sh. 30,000,000 (milioni thelathini). Wachezaji na maofisa walikataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na badala yake walitumia nyumba iliyo nje ya uwanja.

  • Meneja Walter Harson: Amefungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba, Clatous Chama.

  • Shabiki Mohamed Ally Mposo: Amefungiwa kuingia uwanjani kwa miezi 12 kwa kosa la kuingia uwanjani wakati wa mapumziko na kumwaga vimiminika (vitendo vinavyotafsiriwa kama imani za kishirikina).

Mechi: Mtibwa Sugar 0-1 Dodoma Jiji FC (Mechi Na. 154)

  • Dodoma Jiji FC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo (MCM) na kufika wakiwa pungufu ya vifaa na wawakilishi wanaohitajika kikanuni.

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE β†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE β†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE β†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE β†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE β†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE β†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE β†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE β†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE β†’