Mourinho ni suala la muda tu Real Madrid

Joel JJ By Joel JJ • 11th May 2026

Mourinho ni suala la muda tu Real Madrid

Taarifa zinazidi kushika kasi barani Ulaya kuhusu uwezekano wa kocha José Mourinho kurejea ndani ya Real Madrid kwa mara nyingine.

Licha ya Mourinho kujitokeza hadharani na kukanusha kufanya mazungumzo yoyote na viongozi wa Madrid, ripoti mbalimbali kutoka Hispania na Ureno zinaeleza kuwa mawasiliano ya chini kwa chini bado yanaendelea.

Vyombo kadhaa vya habari Ulaya vimeripoti kuwa Rais wa Real Madrid, Florentino Pérez anamtazama Mourinho kama chaguo sahihi la kurejesha nidhamu na ushindani ndani ya kikosi hicho baada ya msimu wenye matokeo yasiyoridhisha.

Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha Benfica, amekuwa akihusishwa vikali na kurejea Santiago Bernabéu, huku baadhi ya ripoti zikidai kuwa tayari viongozi wa Benfica wameanza kutafuta mbadala wake endapo dili hilo litakamilika.

Katika mkutano wake wa hivi karibuni na waandishi wa habari, Mourinho alisema bado hajapigiwa simu na mtu yeyote kutoka Real Madrid na kwamba ataendelea kubaki makini na majukumu yake Benfica hadi mwisho wa msimu.

Hata hivyo, ripoti nyingine zinaeleza kuwa nyuma ya pazia tayari kuna majadiliano yanayoendelea kuhusu uwezekano wa Mourinho kurejea Bernabéu, huku Perez akitajwa kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa kwenye uamuzi huo.

Mourinho aliwahi kuifundisha Real Madrid kati ya mwaka 2010 hadi 2013 ambapo aliipa ubingwa wa La Liga, Copa del Rey pamoja na kuiwezesha kurejea kuwa tishio Ulaya. Kipindi chake kilikumbukwa zaidi kwa ushindani mkubwa dhidi ya FC Barcelona ya wakati huo chini ya Pep Guardiola.

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE →
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE →
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE →
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE →
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE →
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE →
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE →
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE →
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE →
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE →