Local,Normal News,Tanzania, Kenya, Uganda, Pamoja

Droo ya kufuzu Afcon 2027 kufanyika Cairo Jumanne

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 May 2026
Droo ya kufuzu Afcon 2027 kufanyika Cairo Jumanne

Droo ya kupanga makundi ya michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 inatarajiwa kufanyika Jumanne, Mei 19, 2026, katika hafla inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mataifa mbalimbali barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), droo hiyo itaamua mfumo wa makundi yatakayoanza safari ya timu 48 kuelekea fainali za AFCON 2027 zitakazofanyika nchini Kenya, Uganda na Tanzania.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa sherehe hiyo itafanyika Cairo, Misri saa 9 Alasiri, huku maandalizi yakiwa yamekamilika kwa ajili ya kuhakikisha droo inafanyika kwa uwazi na viwango vya juu vya kiutawala kama ilivyo kawaida ya CAF.

Kwa mujibu wa CAF, michuano ya kufuzu itahusisha jumla ya timu 48, ikiwa ni pamoja na mataifa matatu wa wenyeji ambao tayari wamepata nafasi ya moja kwa moja katika fainali. Mfumo huo utatoa nafasi kwa mataifa 24 kufuzu kwenye mashindano ya mwisho.

AFCON 2027 yenyewe itakuwa ya kihistoria kwa Afrika Mashariki, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mataifa matatu Kenya, Uganda na TanzaniaΒ  kushirikiana kuiandaa michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika.

Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027, ambapo maandalizi ya viwanja na miundombinu yameendelea katika nchi zote tatu wenyeji ili kuhakikisha mashindano yanakuwa ya kisasa na yenye viwango vya kimataifa.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
5h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
9h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
10h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
12h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
12h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
18h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
18h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’