Rio Ferdinand atua Tanzania kwa ziara maalum

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th May 2026


Rio Ferdinand atua Tanzania kwa ziara maalum

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, Rio Ferdinand, amewasili nchini Tanzania kwa ziara maalum inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya michezo, maendeleo ya vijana na kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia michezo.

Ziara hiyo imekuja kufuatia mwaliko rasmi kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Paul Makonda ambaye amesema ujio wa Rio Ferdinand ni sehemu ya mkakati mpana wa Serikali wa kufungua fursa kwa vijana wa Kitanzania kupitia michezo na diplomasia ya michezo.

Kwa mujibu wa taarifa, Rio Ferdinand anatarajiwa kuwa nchini kuanzia Mei 19 hadi Mei 22, 2026 ambapo atatembelea maeneo mbalimbali ya michezo, kukutana na wadau wa sekta hiyo pamoja na viongozi wa Serikali.

Katika ujumbe wake wa video uliosambaa mtandaoni, Rio Ferdinand alisema anafurahishwa na mazungumzo aliyofanya na Waziri Makonda kuhusu fursa zilizopo Tanzania katika michezo, utamaduni na maendeleo ya vijana. Pia alieleza kuwa ana hamu ya kujifunza zaidi kuhusu utamaduni wa Tanzania na kuona namna ambavyo michezo inaweza kufungua milango ya mafanikio kwa vijana wengi.

Waziri Makonda amesema Serikali inaendelea kushirikiana na mastaa mbalimbali wa kimataifa katika michezo ili kuongeza ushawishi wa Tanzania duniani, hususan kuelekea matukio makubwa ya michezo kama AFCON 2027. Aidha, ujio wa Rio Ferdinand unaonekana kama hatua nyingine muhimu katika kuimarisha taswira ya Tanzania kama kitovu cha michezo na utalii barani Afrika.

Rio Ferdinand ni mmoja wa mabeki bora kuwahi kutokea katika soka la England na aliwahi kushinda mataji mbalimbali akiwa na Manchester United, ikiwemo Ligi Kuu England na UEFA Champions League. Uzoefu wake mkubwa katika soka la kimataifa unatajwa kuwa chachu kwa vijana wa Kitanzania wanaotamani kufikia kiwango cha juu katika mchezo huo.

Ziara hiyo pia inatarajiwa kuibua fursa mpya za uwekezaji katika michezo, kukuza vipaji vya vijana na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na wadau wa michezo duniani. Wadau wengi wa soka nchini wamepokea ujio huo kwa furaha kubwa wakiamini unaweza kuhamasisha kizazi kipya cha wachezaji wa Tanzania kuamini ndoto zao.


  

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE β†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE β†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE β†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE β†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE β†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE β†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE β†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE β†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE β†’