Local,Transfer News,Tetesi, Azam, Simba

Simba yatajwa kumuwania winga Azam Fc

Joel JJ By Joel JJ
โ€ข
22 May 2026
Simba yatajwa kumuwania winga Azam Fc

Klabu ya Simba SC imeendelea kujipanga kwa ajili ya msimu ujao kwa kufanya usajili wa wachezaji wa ndani, ambapo tayari imekamilisha mpango wa kumsajili beki wa kulia Nathaniel Chilambo kutoka Azam FC.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu, Chilambo ambaye mkataba wake na Azam FC unatarajiwa kumalizika mwezi ujao, tayari amesaini โ€œpre-contractโ€ ya kuitumikia Simba. Inadaiwa kuwa mchezaji huyo amekubali mkataba wa miaka mitatu na Wekundu wa Msimbazi, hatua inayoashiria mwanzo wa maboresho ya kikosi hicho.

Hata hivyo, Simba haijaishia hapo. Klabu hiyo sasa imemuweka kwenye rada winga wa Azam FC, Abdul Suleiman โ€œSopuโ€, ambaye naye mkataba wake unakaribia kufikia ukomo mwezi ujao.

Kama ilivyo kwa Chilambo, Sopu pia anaweza kujiunga na Simba bila ada ya uhamisho endapo mazungumzo yatakamilika baada ya mkataba wake na Azam FC kumalizika.

Sopu ni mchezaji aliyekulia kwenye mfumo wa vijana wa Simba B kabla ya kujiunga na Coastal Union, na baadaye kusajiliwa na Azam FC. Uzoefu huo unamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoeleweka vyema kwenye soka la Tanzania.

Msimu huu, Sopu hakuonekana sana uwanjani kutokana na changamoto za majeraha, lakini kwa sasa ameonekana kurejea fiti na anapambana kurejesha nafasi yake ndani ya kikosi cha Azam FC.

Simba inaonekana kuendelea na mkakati wa kufunga usajili mapema ili kuhakikisha inakuwa tayari kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa rasmi, hatua inayolenga kuimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao.

Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa Simba pia imekaribia kukamilisha usajili wa kiungo Kelvin Nashon kutoka Pamba Jiji FC pamoja na winga Ramadhan Chobwedo kutoka TRA United, ikiwa ni sehemu ya kuongeza kina na ushindani ndani ya timu.

More Stories

Ngorongoro Heroes yatangulia nusu fainali CECAFA U20 kwa kishindo
Ngorongoro Heroes yatangulia nusu fainali CECAFA U20 kwa kishindo
1h ago
READ MORE โ†’
Samatta afunga bao lake la pili, Le Havre ikipoteza
Samatta afunga bao lake la pili, Le Havre ikipoteza
1h ago
READ MORE โ†’
Salah hakamatiki Uturuki, apiga hat-trik Trabzonspor ikiifumua Galatasaray 4-0
Salah hakamatiki Uturuki, apiga hat-trik Trabzonspor ikiifumua Galatasaray 4-0
2h ago
READ MORE โ†’
Azam Fc yaonywa, Yanga yakumbana na faini - Kamati ya saa 72
Azam Fc yaonywa, Yanga yakumbana na faini - Kamati ya saa 72
2h ago
READ MORE โ†’
Mshambuliaji wa zamani Yanga aibukia Zambia
Mshambuliaji wa zamani Yanga aibukia Zambia
2h ago
READ MORE โ†’
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
10h ago
READ MORE โ†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
14h ago
READ MORE โ†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
15h ago
READ MORE โ†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
17h ago
READ MORE โ†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
17h ago
READ MORE โ†’