International,Normal News,Manchester United, Premier League

Bruno Fernandez atangazwa kuwa mchezaji bora wa EPL 25/26

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
23 May 2026
Bruno Fernandez atangazwa kuwa mchezaji bora wa EPL 25/26

Bruno Fernandes ametangazwa rasmi kuwa Mchezaji Bora wa Premier League kwa msimu wa 2025/26 baada ya msimu wa kiwango cha juu uliomfanya kuwa moyo wa Manchester United. Nahodha huyo wa United amepewa tuzo ya EA Sports FC Player of the Season kufuatia mchango mkubwa alioutoa katika kampeni iliyowarudisha United kwenye UEFA Champions League.

Bruno anakamilisha msimu akiwa mpaka sasa amecheza mechi 34 za ligi, akifunga mabao 8 na kutoa asisti 20, idadi iliyoweka rekodi mpya katika historia ya Premier League. Jumla ya michango yake 28 ya magoli imekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya United msimu huu, hasa katika kipindi ambacho timu ilipitia changamoto nyingi ndani na nje ya uwanja.

Mbali na asisti hizo za kihistoria, Bruno ametawala karibu kila takwimu muhimu ya ubunifu katika ligi. Ameongoza kwa expected assists nyingi zaidi, nafasi nyingi zilizotengenezwa, big chances nyingi zilizoundwa, pamoja na pasi nyingi sahihi ndani ya eneo la hatari. Kwa kifupi, karibu kila eneo la ubunifu wa mashambulizi lilikuwa chini ya jina lake msimu huu.

Kilichofanya msimu wake kuwa wa kipekee zaidi ni ukweli kwamba alifanya yote hayo wakati United wakipitia msimu wenye presha kubwa. Kulikuwa na mabadiliko ya kocha, matokeo yaliyotikisa timu mara kadhaa, na kipindi ambacho mashabiki walikuwa na mashaka kuhusu mustakabali wa klabu. Lakini Bruno aliendelea kuwa nguzo ya timu, akiongoza kwa kiwango na mfano wa uwanjani.

Katika umri wa miaka 31, wengi walikuwa wanaanza kuhoji kama bado ana uwezo wa kucheza katika kiwango chake cha juu. Badala ya kupungua, ameonekana kuwa bora zaidi. Rekodi ya asisti 20 imeweka jina lake mbele ya majina makubwa yaliyowahi kucheza Premier League kama Thierry Henry, Kevin De Bruyne na Cesc FΓ bregas, Huku yeye akiwa amebakisha mchezo mmoja dhidi ya Brighton.

Kwa Manchester United, msimu huu utaendelea kukumbukwa kama msimu wa kurejea kwenye ushindani wa juu, na jina la Bruno Fernandes litabaki katikati ya hadithi hiyo. Kutoka kuwa nahodha mwenye kupingwa hadi kuwa mchezaji bora wa ligi nzima, Bruno amethibitisha kuwa bado ni mmoja wa viungo bora zaidi duniani.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
3h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
8h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
8h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
10h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
10h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
16h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
17h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’