Local,Normal News,Ligi Kuu, Simba, Dodoma Jiji, JKT, Mtibwa, TRA, Fountain

Simba yarudi kileleni baada ya ushindi dhidi ya Dodoma Jiji

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 May 2026
Simba yarudi kileleni baada ya ushindi dhidi ya Dodoma Jiji

Mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara zimeendelea kushika kasi leo Jumapili, Mei 24, 2026 huku michezo kadhaa ikipigwa katika viwanja tofauti nchini na kuleta mabadiliko muhimu kwenye msimamo wa ligi.

Ushindi mwembamba wa Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, umerejesha Wekundu wa Msimbazi kileleni mwa msimamo wa ligi. Simba walishinda bao 1-0 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha pointi 58.

Bao pekee la mchezo lilifungwa na mshambuliaji Elie Mpanzu aliyemalizia mpira uliotemwa na kipa wa Dodoma Jiji baada ya Clatous Chama kupiga mkwaju wa penalti. Ushindi huo unaendelea kuongeza presha katika mbio za ubingwa huku Simba wakiendelea kuchuana na watani zao Yanga ambao watashuka dimbani Jumatatu kuikabili Namungo FC.

Katika mchezo mwingine uliopigwa mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar FC walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya JKT Tanzania. JKT Tanzania walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Paul Kasunda dakika ya 19 kabla ya Haroun Lyawatwa kusawazisha kwa Mtibwa dakika ya 37. Kasunda aliifungia tena JKT bao la pili dakika ya 42 na kuwapa wageni uongozi wa muda kabla Mtibwa kusawazisha katika kipindi cha pili na kuokoa pointi moja muhimu nyumbani.

Nayo Fountain Gate FC iliendeleza matokeo mazuri baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TRA United katika mchezo uliochezwa Arusha. Ushindi huo umeipa Fountain Gate matumaini mapya ya kujinasua na kuongeza ushindani katikati ya msimamo wa ligi.

TRA United ni kama wamevuruga hesabu zao kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya nne baada ya kupoteza mchezo huo muhimu nyumbani.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
5h ago
READ MORE β†’
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
10h ago
READ MORE β†’
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
10h ago
READ MORE β†’
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
12h ago
READ MORE β†’
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
13h ago
READ MORE β†’
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
18h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
19h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’