Rupia mbioni kurejea Polisi Fc Kenya

Joel JJ By Joel JJ
โ€ข
10 Jun 2026
Rupia mbioni kurejea Polisi Fc Kenya

Mshambuliaji raia wa Kenya, Elvis Rupia, anaripotiwa kuwa katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kurejea katika klabu yake ya zamani ya Kenya Police FC, ikiwa ni katika harakati za klabu hiyo kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu unaoendelea.

Taarifa kutoka Kenya zinaeleza kuwa mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu nchini humo wamemweka Rupia kama moja ya vipaumbele vyao katika dirisha la usajili, wakiamini anaweza kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji.

Hata hivyo, Kenya Police FC hawako peke yao katika kinyangโ€™anyiro hicho, kwani klabu nyingine kubwa nchini humo, AFC Leopards pia inaripotiwa kumfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji huyo, hali inayoongeza ushindani wa kumsajili.

Sababu kubwa ya Kenya Police FC kuharakisha mazungumzo ni kutokana na uwezekano wa nyota wao wa sasa, Yves Koutiam, kuondoka kuelekea klabu ya Tanzania, Yanga SC. Koutiam, ambaye alijiunga na Police FC Januari 2026 akitokea USFA Ouagadougou, amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu baada ya kufunga mabao 10 katika Ligi Kuu ya Kenya msimu wa 2025โ€“2026.

Rupia, amekuwa na historia ndefu na ya kuvutia katika soka la Afrika Mashariki. Akiwa na Polisi Fc msimu wa 2022โ€“2023, alionesha kiwango cha juu cha ufungaji, ambapo alifunga jumla ya mabao 27 katika ligi kuu ya Kenya, akivunja rekodi iliyodumu kwa zaidi ya miongo minne.

Katika msimu wake wa kwanza baada ya kuhamia Tanzania, Rupia alipitia changamoto kabla ya kupata utulivu, akicheza katika kikosi cha Singida Fountain Gate, ambapo kwa jumla alifunga mabao sita katika msimu mzima.

Msimu wa 2024โ€“2025 ulikuwa bora zaidi kwake akiwa Tanzania, ambapo alichangia mabao 12 kwa jumla, akifunga 10 na kutoa pasi mbili za mwisho, akiwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa katika kikosi chake.

Hata hivyo, msimu wa 2025โ€“2026 umekuwa na changamoto zaidi kwake, ambapo hadi sasa amefunga mabao matatu, likiwemo bao muhimu la sare ya 1โ€“1 dhidi ya Mashujaa FC mwezi Aprili 2026.

Kwa sasa, taarifa zinaeleza kuwa Rupia si sehemu ya kikosi cha Singida Black Stars baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake, jambo linalomuweka huru kuamua hatma ya maisha yake ya soka.

ADVERTISE HERE

More Stories

Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4m ago
READ MORE โ†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
56m ago
READ MORE โ†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE โ†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE โ†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE โ†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE โ†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE โ†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE โ†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE โ†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon dโ€™Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon dโ€™Or
21h ago
READ MORE โ†’