Ligi Kuu ya NBC inaelekea ukiongoni leo mechi mbili mzunguuko wa 27 zikitarajiwa kupigwa.
Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc wako mkoani Mbeya ambapo leo watakuwa uwanjani mechi ya mapema saa 8.
Watakuwa wageni wa Mbeya City katika mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Kama Simba itashinda mchezo huo basi itapanda kileleni mwa msimamo wa ligi kuwaombea 'njaa' watani zao Yanga ili wapoteze mchezo dhidi ya Fountain Gate hapo kesho.
Hapa hivi Mbeya City nao wanazihitaji alama tatu ili kujinusuru na janga la kushuka daraja linalowanyemelea.
Singida BS itachuana na majirani zao Dodoma Jiji katika mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 jioni uwanja wa Airtel, Singida.




