Local,Normal News,TPLB, Simba, Yanga, Azam

Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72

Joel JJ By Joel JJ
β€’
18 Jun 2026
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Juni 16, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatazo;

Ligi Kuu ya NBC

Mechi Namba 203: Mbeya City FC 1-0 Mtibwa Sugar

  • Klabu ya Mtibwa Sugar imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la wachezaji na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi kuonekana wakifanya kitendo kinachoashiria imani za kishirikina kuelekea mchezo tajwa hapo juu.

  • Wachezaji hao na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi walijikusanya katikati ya uwanja na kuweka duara kuashiria kuomba dua lakini mmoja kati ya viongozi alionekana akichimbia vitu chini.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

  • Mwamuzi wa kati mchezo tajwa hapo juu, Liston Hiari kutoka Dar es Salaam ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kuonesha mapungufu ya kiuchezeshaji yaliyotokana na kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Mechi Namba 205: Mashujaa FC 0-2 Young Africans SC

  • Shabiki wa klabu ya Young Africans aliyetambulika kwa jina la Said Selemani Ally amefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi 12, kwa kosa la kuingia kwenye eneo la kuchezea siku moja kabla ya mchezo baada ya Young Africans kumaliza mazoezi yao ya mwisho na kumwaga vitu vyenye asili ya kimiminika na udongo kutokea goli la kusini kuelekea katikati ya uwanja kitendo kilichotafsiriwa kama imani za kishirikina.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 47:2 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa klabu.

Mechi Namba 205: Simba SC 2-1 Pamba Jiji FC

  • Mwamuzi wa kati Hance Mabena kutoka Tanga na Mwamuzi msaidizi namba moja (1) Frank Komba wa mchezo tajwa hapo juu, wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa makosa la kuonesha mapungufu ya kiuchezeshaji yaliyotokana na kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

  • Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. Milioni kumi (10,000,000) kwa kosa la mashabiki wake kumwagia maji mwamuzi msaidizi namba moja (1) wakipinga maamuzi ya mwamuzi huyo mara baada ya kunyoosha kibendera kuashiria mchezaji wa Simba kuotea.

  • Hili ni kosa la kujirudia kwa mashabiki wa klabu ya Simba ndani ya msimu huu wa 2025/2026, wakitenda kosa mfanano wa hilo katika michezo mitatu tofauti na kusababisha klabu kuadhibiwa.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

  • Klabu ya Pamba Jiji imetozwa faini ya Sh. Laki tano (500,000) kwa kosa la wachezaji wake sita (6) kuonyeshwa kadi za njano.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 47:10 kuhusu udhibiti kwa klabu.

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
41m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
53m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’