Makocha Simba, Coastal Union wafunguka maandalizi nusu fainali CRDB Cup

Joel JJ By Joel JJ • 19th June 2026


Makocha Simba, Coastal Union wafunguka maandalizi nusu fainali CRDB Cup

Makocha wa timu za Simba SC na Coastal Union wamezungumza kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Kombe la CRDB utakaopigwa Jumamosi, Juni 20 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mkoani Arusha, huku kila upande ukionesha kujiamini na maandalizi makini.

SIMBA YAAHIDI MAPAMBANO MAKALI NUSU FAINALI

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema kikosi chake kipo tayari kwa mtihani huo mgumu dhidi ya Coastal Union, akisisitiza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatinga hatua ya fainali ya mashindano hayo ya taifa.

Barker alisema Simba inatambua ubora wa mpinzani wao, lakini maandalizi yao yamejikita katika kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

“Tumejiandaa vyema na tupo tayari kwa mchezo huu wa nusu fainali Kombe la CRDB. Tunatambua ubora na ugumu wa Coastal Union. Mara ya mwisho tulipokutana nao Mkwakwani tulilazimika kutoka nyuma kupata ushindi,” alisema Barker.

Aliongeza kuwa kikosi chake kiko tayari kuonesha kiwango bora zaidi ili kufanikisha lengo la kufika fainali.

COASTAL UNION: TUNAHESHIMU SIMBA, LAKINI TUNAPAMBANA

Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu wa Coastal Union, Fikiri Elias, amesema mchezo huo ni wa mtoano na si wa ligi, hivyo kila kitu kinaweza kutokea uwanjani.

Amesema timu yake imejipanga kimkakati na inajua ugumu wa mchezo huo, lakini inalenga kufanya vizuri na kufuzu fainali.

“Tunakwenda kushiriki mchezo wa mtoano na si ligi kuu, lazima mmoja apite kwenda fainali. Tumejipanga vizuri kimbinu, ingawa tunajua mchezo utakuwa mgumu sana,” alisema Elias.

Ameongeza kuwa historia ya mechi zilizopita dhidi ya Simba imekuwa fundisho kwao, na sasa wamejipanga kuonesha tofauti uwanjani.

“Historia ipo ili tujifunze, tumejifunza kwenye michezo iliyopita tuliyocheza dhidi ya Simba, kesho ndio mtaona tulichojifunza,” alisisitiza.


  

More Stories

Himid aongeza mwaka Azam Fc
Himid aongeza mwaka Azam Fc
Today, READ MORE →
Kone kuuguza majeraha kwa miezi 6
Kone kuuguza majeraha kwa miezi 6
Today, READ MORE →
Makocha Simba, Coastal Union wafunguka maandalizi nusu fainali CRDB Cup
Makocha Simba, Coastal Union wafunguka maandalizi nusu fainali CRDB Cup
Today, READ MORE →
Ni Wikiendi ya kusaka wanafainali CRDB Cup
Ni Wikiendi ya kusaka wanafainali CRDB Cup
Today, READ MORE →
Ratiba ya Ligi Kuu ya Premia 2026/27 hadharani
Ratiba ya Ligi Kuu ya Premia 2026/27 hadharani
Today, READ MORE →
Ni kweli Real Madrid ilimtaka Alvarez?
Ni kweli Real Madrid ilimtaka Alvarez?
Today, READ MORE →
Canada yaichapa Qatar 6-0, yaandika historia Kombe la Dunia 2026
Canada yaichapa Qatar 6-0, yaandika historia Kombe la Dunia 2026
Today, READ MORE →
Foutain Gate 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Foutain Gate 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Today, READ MORE →
Pamba Jiji 4-0 Mtibwa Sugar, Ligi Kuu
Pamba Jiji 4-0 Mtibwa Sugar, Ligi Kuu
Today, READ MORE →
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE →