International,Normal News,World Cup, Canada, Local

Kone kuuguza majeraha kwa miezi 6

Joel JJ By Joel JJ
19 Jun 2026
Kone kuuguza majeraha kwa miezi 6

Timu ya Taifa ya Canada imepata pigo kubwa baada ya kiungo wake nyota, Ismael Koné (24), kupata majeraha mabaya yatakayomuweka nje ya uwanja kwa takribani miezi sita.

Koné alipata majeraha hayo baada ya kuchezewa rafu mbaya na kiungo wa Qatar, Assim Madibo, katika mchezo wa Kombe la Dunia uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa madaktari wa timu, mchezaji huyo amevunjika mifupa ya tibia na fibula, ambayo ni mifupa muhimu inayounganisha goti na kifundo cha mguu. Kutokana na ukubwa wa majeraha hayo, Koné anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kabla ya kuanza safari yake ya kupona.

Licha ya tukio hilo la kusikitisha, Canada iliendelea kuonyesha kiwango bora uwanjani. Dakika 10 tu baada ya Koné kutolewa nje kwa majeraha, kiungo aliyeingia kuchukua nafasi yake, Nathan Saliba, aliifungia Canada bao la nne.

Saliba aliwagusa mashabiki wengi kwa namna alivyosherehekea bao hilo, ambapo aliinua juu jezi namba 8 ya Koné kama ishara ya kumuunga mkono mwenzake aliyepata majeraha.

Hata hivyo, majonzi ya kuumia kwa Koné hayakuzuia Canada kuandika historia. Ushindi wao wa mabao 6-0 uliwapa furaha kubwa ya kupata ushindi wao wa kwanza wa kihistoria katika Kombe la Dunia 2026.

More Stories

Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
Barcelona yaendeleza kichapo Laliga ikimfunga Sevilla, Raphinha hashikiki.
4h ago
READ MORE →
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
Mamelodi Sundowns yaibuka kidedea mbele ya Al Ahli
8h ago
READ MORE →
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
Arsenal yaduwazwa 3-0 na Brighton
9h ago
READ MORE →
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
11h ago
READ MORE →
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
11h ago
READ MORE →
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
15h ago
READ MORE →
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
17h ago
READ MORE →
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
17h ago
READ MORE →
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
1d ago
READ MORE →
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE →