Ni Wikiendi ya kusaka wanafainali CRDB Cup

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th June 2026

Ni Wikiendi ya kusaka wanafainali CRDB Cup

Hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB imewadia huku timu nne zikisaka nafasi ya kutinga fainali ya mashindano hayo.

Pambano la kwanza litapigwa Jumamosi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, ambapo Simba SC itavaana na Coastal Union kuwania tiketi ya kwenda fainali.

Macho ya wengi yataelekezwa jijini Mwanza Jumapili katika Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo Azam FC itakuwa na kibarua kizito dhidi ya Yanga SC katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu hizo mbili.

Timu zitakazofanikiwa kushinda mechi zao zitakutana fainali kuwania taji la CRDB Federation Cup na nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mashabiki wa soka nchini wanatarajia wikendi yenye ushindani mkali, burudani na vita ya kutafuta tiketi ya fainali.

More Stories

Himid aongeza mwaka Azam Fc
Himid aongeza mwaka Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Kone kuuguza majeraha kwa miezi 6
Kone kuuguza majeraha kwa miezi 6
Today, READ MORE β†’
Makocha Simba, Coastal Union wafunguka maandalizi nusu fainali CRDB Cup
Makocha Simba, Coastal Union wafunguka maandalizi nusu fainali CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Wikiendi ya kusaka wanafainali CRDB Cup
Ni Wikiendi ya kusaka wanafainali CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ratiba ya Ligi Kuu ya Premia 2026/27 hadharani
Ratiba ya Ligi Kuu ya Premia 2026/27 hadharani
Today, READ MORE β†’
Ni kweli Real Madrid ilimtaka Alvarez?
Ni kweli Real Madrid ilimtaka Alvarez?
Today, READ MORE β†’
Canada yaichapa Qatar 6-0, yaandika historia Kombe la Dunia 2026
Canada yaichapa Qatar 6-0, yaandika historia Kombe la Dunia 2026
Today, READ MORE β†’
Foutain Gate 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Foutain Gate 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Today, READ MORE β†’
Pamba Jiji 4-0 Mtibwa Sugar, Ligi Kuu
Pamba Jiji 4-0 Mtibwa Sugar, Ligi Kuu
Today, READ MORE β†’
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yesterday, READ MORE β†’