International,Normal News,World Cup, Tunisia, Japan, Local

Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Jun 2026
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan

Ndoto za Tunisia katika Kombe la Dunia 2026 zimefikia tamati kwa njia ya kusikitisha baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Japan katika mchezo wa Kundi F uliochezwa leo Jumapili Juni 21.

Matokeo hayo yameiacha Tunisia mkiani mwa kundi hilo huku ikipoteza mechi yake ya pili mfululizo, baada ya awali kufungwa mabao 5-1 na Sweden. Kipigo cha Japan kimeifanya timu hiyo kuruhusu mabao tisa katika mechi mbili, jambo linaloonyesha udhaifu mkubwa wa safu yao ya ulinzi.

Japan ilianza mchezo kwa kasi kubwa na kutawala umiliki wa mpira tangu dakika za mwanzo. Mashambulizi ya mara kwa mara yaliwalazimisha Watunisia kucheza muda mwingi katika eneo lao la hatari huku safu ya ulinzi ikionekana kuzidiwa na kasi na mbinu za wapinzani wao.

Daichi Kamada alifunga bao la kwanza dakika ya nne huku Ayase Ueda akifunga mabao mawili na Junya Ito akifunga bao la nne. Tunisia ilijaribu kujibu kupitia mipira ya kushtukiza lakini ilishindwa kuunda nafasi za kutosha za kuisumbua safu ya ulinzi ya Japan.

Kipigo hicho kinaifanya Japan kuimarisha nafasi yake ya kufuzu hatua ya 16 bora huku Tunisia ikibaki bila pointi yoyote baada ya michezo miwili.

Mashabiki wa Tunisia walionekana kuvunjika moyo baada ya kipenga cha mwisho huku wengi wakiamini timu yao haikuonyesha kiwango kinachostahili katika mashindano hayo makubwa. Kuaga kwa namna hii kunakuwa pigo kubwa kwa taifa hilo ambalo lilikuwa na matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika michuano ya mwaka huu.

Tunisia hawakuwa wameruhusu bao lolote kwenye hatua ya kufuzu ambapo katika mechi 10, walishinda tisa na kutoka droo mchezo mmoja. Hata hivyo sasa wamepigwa mabao 9 kwenye mechi mbili tu

More Stories

Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
3h ago
READ MORE β†’
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
5h ago
READ MORE β†’
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
5h ago
READ MORE β†’
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
20h ago
READ MORE β†’
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE β†’
Kocha Dimitar Pantev ateuliwa kuwa kocha mpya wa Richard Bay.
Kocha Dimitar Pantev ateuliwa kuwa kocha mpya wa Richard Bay.
1d ago
READ MORE β†’
Sandaland kuchukua hatua kufuatia kauli za Makonda juu ya jezi za Taifa stars
Sandaland kuchukua hatua kufuatia kauli za Makonda juu ya jezi za Taifa stars
1d ago
READ MORE β†’
Tuchel awarejesha Trent na Palmer kikosi cha England
Tuchel awarejesha Trent na Palmer kikosi cha England
1d ago
READ MORE β†’
Wizara kuunda kamati kuchunguza mkataba wa jezi timu za taifa
Wizara kuunda kamati kuchunguza mkataba wa jezi timu za taifa
1d ago
READ MORE β†’
Pyramids ya mokwena haishikiki misri, yaandelea kuongoza msimamo
Pyramids ya mokwena haishikiki misri, yaandelea kuongoza msimamo
1d ago
READ MORE β†’