International,Transfer News,Liverpool, Leipzig, Local

Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande

Joel JJ By Joel JJ
21 Jun 2026
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande

Liverpool FC inaendelea kuonyesha nia ya dhati kumsajili nyota chipukizi wa RB Leipzig RB Leipzig, Yan Diomande, baada ya ofa yao ya awali ya takribani €100 milioni kukataliwa na klabu hiyo ya Ujerumani.

Kwa mujibu wa taarifa,  Liverpool sasa inajiandaa kuwasilisha ofaa mpya iliyoboreshwa ili kuvunja pingamizi la Leipzig na kuingia hatua ya juu ya mazungumzo. 

Leipzig wagoma kumuuza Diomande

RB Leipzig imeendelea kusisitiza kuwa haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo kwa sasa, ikipendelea kumbakiza kwa angalau msimu mmoja zaidi. Hata hivyo, inaripotiwa kuwa Diomande mwenyewe anaonyesha utayari wa kuondoka endapo makubaliano yatafikiwa kati ya vilabu. 

Klabu hiyo ya Bundesliga inaaminika kuweka thamani ya mchezaji huyo kati ya €100M hadi €120M+, kutokana na kiwango chake kilichopanda kwa kasi na mchango wake mkubwa ndani ya kikosi. 

PSG nao ndani ya kinyang’anyiro

Mbali na Liverpool, mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG) nao wanatajwa kuwa wanafuatilia kwa karibu mchakato wa uhamisho huo nyuma ya pazia.

Diomande kwa sasa yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kinachoshiriki michuano ya kombe la Dunia inayoendelea Mexico, Canada na Marekani.

More Stories

Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
Nyota Stars waingia kambini tayari kwa mechi za kufuzu Afcon 2027
36m ago
READ MORE →
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
Simba kujichimbia Afrika Kusini kujiandaa na Kariakoo Derby
50m ago
READ MORE →
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
Madrid Derby: Atletico na Real kwenye vita ya majirani
4h ago
READ MORE →
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
Hii hapa rekodi tamu ya Barker Ligi Kuu
6h ago
READ MORE →
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
Sundowns kuchuana na Al Ahli katika vita ya Afrika na Asia
7h ago
READ MORE →
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
Ft: Yanga 1-0 St George, Yanga yapata ushindi mechi ya kirafiki.
21h ago
READ MORE →
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
Dockers Derby yarudi baada ya miaka 14, Ulinzi wa London ukiimarishwa.
1d ago
READ MORE →
Kocha Dimitar Pantev ateuliwa kuwa kocha mpya wa Richard Bay.
Kocha Dimitar Pantev ateuliwa kuwa kocha mpya wa Richard Bay.
1d ago
READ MORE →
Sandaland kuchukua hatua kufuatia kauli za Makonda juu ya jezi za Taifa stars
Sandaland kuchukua hatua kufuatia kauli za Makonda juu ya jezi za Taifa stars
1d ago
READ MORE →
Tuchel awarejesha Trent na Palmer kikosi cha England
Tuchel awarejesha Trent na Palmer kikosi cha England
1d ago
READ MORE →