Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st June 2026


Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali

Azam FC imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kudumu kwa dakika 120.

Mchezo huo ulikuwa wa kusisimua kutoka mwanzo hadi mwisho huku ukishuhudia mabingwa watetezi Yanga wakiondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kutawala kwa miaka minne mfululizo.

Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Himid Mao aliyefunga kwa kichwa kufuatia uzembe wa mabeki wa Yanga kushindwa kuondoa hatari ndani ya eneo la penalti. Bao hilo liliwapa Azam FC uongozi wa 1-0 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Yanga walirejea kwa nguvu na kufanikiwa kusawazisha kupitia mshambuliaji Prince Dube aliyemalizia kwa kichwa krosi safi ya Allan Okello.

Hata hivyo, makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga yaliendelea kuwagharimu baada ya Lameck Lawi kuifungia Azam FC bao la pili dakika ya 85 kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Feisal Salum.

Dakika tatu baadaye, nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto aliwarejesha mchezoni Wananchi kwa kufunga bao la kusawazisha kwa kichwa akitumia tena krosi ya Allan Okello na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Matokeo hayo yalipeleka mchezo katika dakika 30 za nyongeza ambapo Yanga walionekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda hasa baada ya Azam FC kubaki na wachezaji 10 kufuatia beki Yoro Diaby kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumuangusha Prince Dube akiwa katika nafasi ya wazi ya kufunga.

Licha ya Yanga kushambulia mara kwa mara, kipa wa Azam FC Zuberi Foba alikuwa mwiba kwa kufanya saves muhimu zilizoendelea kuiweka timu yake salama.

Dakika za mwisho za muda wa nyongeza zilileta pigo kubwa kwa Yanga baada ya beki Bacca kufanya kosa la pasi ya kurudisha nyuma. Mshambuliaji Japhet Kitambala aliuwahi mpira huo na kufunga bao la ushindi lililoihakikishia Azam FC tiketi ya fainali kwa ushindi wa mabao 3-2.

Kwa ushindi huo, Azam FC sasa itakutana na Simba SC katika fainali ya CRDB Federation Cup, mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kati ya vigogo hao wa soka la Tanzania. Simba SC walikuwa tayari wamekata tiketi ya fainali baada ya kushinda nusu fainali yao dhidi ya Coastal Union.

Kwa upande wa Yanga, ndoto ya kutetea taji lao imefikia mwisho baada ya kutwaa kombe hilo kwa misimu minne mfululizo. Sasa Wananchi wataelekeza nguvu zao katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga na Azam FC wanatarajiwa kukutana tena Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu ambao unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mbio za ubingwa.


  

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE β†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE β†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE β†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE β†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE β†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE β†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE β†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE β†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE β†’