Je, fainali ya Kombe la Shirikisho itarejea Dar es salaam?

Jairo Mtitu By Jairo Mtitu β€’ 22nd June 2026

Je, fainali ya Kombe la Shirikisho itarejea Dar es salaam?

Baada ya Simba SC na Azam FC kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank msimu wa 2025/26, mjadala mkubwa sasa umehamia kwenye uwanja utakaotumika kuchezwa pambano hilo la Julai 4, 2026.

Kwa misimu miwili mfululizo, fainali hiyo imefanyika Zanzibar katika dimba la New Amaan Complex, lakini safari hii wadau wengi wa soka wanaona ni wakati muafaka wa kuirejesha Dar es Salaam, jiji ambalo halijashuhudia fainali hiyo tangu msimu wa 2015/16.

Kutokana na maboresho yanayoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, viwanja vingine kama Uhuru Stadium na Azam Complex vinatajwa kuwa miongoni mwa chaguo zinazoweza kuandaa mchezo huo mkubwa unaotarajiwa kuvuta maelfu ya mashabiki.

Mikoa iliyowahi kuwa mwenyeji wa fainali ya Kombe la Shirikisho tangu 2015/16:

2015/16 – Dar es Salaam (Benjamin Mkapa)

2016/17 – Dodoma (Jamhuri Stadium)

2017/18 – Arusha (Sheikh Amri Abeid Stadium)

2018/19 – Lindi (Ilulu Stadium)

2019/20 – Rukwa (Nelson Mandela Stadium – Sumbawanga)

2020/21 – Kigoma (Lake Tanganyika Stadium)

2021/22 – Arusha (Sheikh Amri Abeid Stadium)

2022/23 – Tanga (Mkwakwani Stadium)

2023/24 – Zanzibar (New Amaan Complex)

2024/25 – Zanzibar (New Amaan Complex) Huku

TFF ikiwa bado haijatangaza rasmi venue ya fainali ya mwaka huu, macho na masikio ya mashabiki yameelekezwa kwenye uamuzi huo muhimu ambao utaamua mkoa gani utaandika historia nyingine ya mashindano hayo.

More Stories

Je, fainali ya Kombe la Shirikisho itarejea Dar es salaam?
Je, fainali ya Kombe la Shirikisho itarejea Dar es salaam?
Today, READ MORE β†’
Serengeti Boys Warejea Mzigoni
Serengeti Boys Warejea Mzigoni
Today, READ MORE β†’
Arusha yazidi kunoga, uwanja wa AFCON 2027 wachukua sura mpya
Arusha yazidi kunoga, uwanja wa AFCON 2027 wachukua sura mpya
Today, READ MORE β†’
IRAN : Taifa Linalopigana Ndani Na Nje Ya Uwanja
IRAN : Taifa Linalopigana Ndani Na Nje Ya Uwanja
Today, READ MORE β†’
Yanga Watafuta Majibu Ya Azam Zanzibar
Yanga Watafuta Majibu Ya Azam Zanzibar
Today, READ MORE β†’
Yanga sasa wana jukumu moja tu: Kulinda alama mbili Ligi Kuu
Yanga sasa wana jukumu moja tu: Kulinda alama mbili Ligi Kuu
Today, READ MORE β†’
Argentina na Austria kukutana kwa mara ya kwanza kihistoria kwenye mechi ya kimashindano
Argentina na Austria kukutana kwa mara ya kwanza kihistoria kwenye mechi ya kimashindano
Today, READ MORE β†’
Misri yaitandika New Zealand 3-1 yakaribia kufuzu 32 bora
Misri yaitandika New Zealand 3-1 yakaribia kufuzu 32 bora
Today, READ MORE β†’
Cape Verde yaikomalia Uruguay yapata sare ya pili
Cape Verde yaikomalia Uruguay yapata sare ya pili
Today, READ MORE β†’
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Yesterday, READ MORE β†’