Uchawi wa Ghana ulivyofanya kazi kwa Waingereza

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 24th June 2026


Uchawi wa Ghana ulivyofanya kazi kwa Waingereza

Timu ya Taifa ya Ghana imeendelea kuonyesha uimara wake katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya England katika mchezo ulioshuhudia Waingereza wakitawala kwa kiasi kikubwa bila kupata njia ya kutikisa nyavu.

England walitengeneza nafasi nyingi za kufunga katika dakika zote 90, lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo mbele ya lango la Ghana. Nahodha na mshambuliaji wao tegemeo, Harry Kane, alishindwa kupata bao licha ya kupata nafasi kadhaa za kuifungia timu yake.

Kwa upande wa Ghana, kipa Benjamin Asare alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuokoa mashambulizi mengi hatari na kuhakikisha timu yake inaondoka na pointi muhimu. Uimara wake chini ya milingoti uliwapa wakati mgumu washambuliaji wa England ambao walionekana kukosa majibu dhidi ya kiwango chake bora.

Mashabiki wengi wa Ghana walitania kuwa β€œuchawi wa mganga wao” umeendelea kufanya kazi, baada ya timu hiyo kufanikiwa kuhimili presha kubwa ya England kwa dakika zote za mchezo na kuondoka bila kuruhusu bao.

Matokeo hayo yameifanya Ghana kuandika clean sheet yake ya pili katika Kombe la Dunia 2026, jambo linaloonyesha uimara mkubwa wa safu yao ya ulinzi na nidhamu ya kiuchezaji ambayo imekuwa moja ya silaha zao muhimu katika mashindano haya.

Licha ya kumiliki mpira na kutawala mchezo kwa muda mwingi, England walishindwa kupata ushindi waliouhitaji, huku Ghana wakiondoka kifua mbele baada ya kuzuia moja ya safu hatari zaidi za ushambuliaji katika soka la kimataifa.


  

More Stories

Leo Tunaharibu mipango Yao ; KIFARU
Leo Tunaharibu mipango Yao ; KIFARU
Today, READ MORE β†’
Wachezaji wa Burkina Faso wapigwa msasa wa uzalendo jeshini
Wachezaji wa Burkina Faso wapigwa msasa wa uzalendo jeshini
Today, READ MORE β†’
Xabi Alonso Apata Usajili Wake wa Kwanza, ni Marco Palestra
Xabi Alonso Apata Usajili Wake wa Kwanza, ni Marco Palestra
Today, READ MORE β†’
Yanga, Azam Mikononi mwa Arajiga
Yanga, Azam Mikononi mwa Arajiga
Today, READ MORE β†’
ANARUDI : Brazil inapumua , Scotland inaomba Mungu
ANARUDI : Brazil inapumua , Scotland inaomba Mungu
Today, READ MORE β†’
Uchawi wa Ghana ulivyofanya kazi kwa Waingereza
Uchawi wa Ghana ulivyofanya kazi kwa Waingereza
Today, READ MORE β†’
Ronaldo aweka rekodi kombe la Dunia
Ronaldo aweka rekodi kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Colombia ya Iduaza Congo Drc na Kutinga hatua ya mtoano
Colombia ya Iduaza Congo Drc na Kutinga hatua ya mtoano
Today, READ MORE β†’
Nkeng atajwa kuwa mbadala wa Sowah Simba
Nkeng atajwa kuwa mbadala wa Sowah Simba
Today, READ MORE β†’
Uganda Mabingwa Cecafa U17 Kwa Wanawake
Uganda Mabingwa Cecafa U17 Kwa Wanawake
Today, READ MORE β†’