Mabao mawili aliyofunga mshambuliaji wa Singida Black Stars Ndumumwe Mossi kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons jana yamemfanya afikishe mabao 14 sasa akimfikia Feisal Salum 'Fei Toto'.
Mossi aliyetua Singida BS kwenye usajili wa dirisha dogo, amekuwa shujaa wa Singida BS na kuifanya timu hiyo ijihakikishie ushiriki wa michuano ya kombe la Shirikisho (CAFCC) msimu ujao.
Wakati Mossi na Fei Toto wakichuana kileleni, Allan Okello (Yanga), Mathew Tegisi (Pamba Jiji) na Fabrice Ngoy (Namungo Fc) wanafuatia kila mmoja akiwa amefunga mabao 11.
Suleiman Mwalimu wa Simba yeye anaongoza kwa upande wa Wekundu hao wa Msimbazi akiwa amefunga mabao 9 akiwa sawa na nyota wa Yanga Prince Dube, Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya.
Kuelekea mechi mbili za kuhitimisha msimu, ni wazi Fei Toto na Mossi wako katika nafasi nzuri zaidi ya kuibuka na tuzo hiyo.




