Klabu ya Yanga SC imeanza rasmi harakati za kumrejesha kiungo mshambuliaji wake wa zamani, Stephane Aziz Ki, kutoka klabu ya Al Ittihad, imefahamika.
Kwa mujibu wa taarifa, Yanga SC tayari imetuma ofa rasmi kwa Al Ittihad ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumrudisha nyota huyo ambaye aliwahi kuwa MVP wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 kabla ya kutimkia Morocco kujiunga na Wydad CA.





