Baada ya kukamilika kwa mechi za mzunguuko wa 28, unaweza kusema klabu za Yanga, Simba, Azam Fc na Singida BS tayari zimejihakikishia tiketi ya kushiriki mashindano ya CAF msimu ujao 2026/27.
Ushindi wa mabao 3-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Azam Fc umewafanya wafikishe alama 69 ambazo ni Simba pekee inayoweza kuzifikia katika mechi zilizobaki.





