Simba dhidi ya Singida BS kupigwa dimba la Isamuhyo

Joel JJ By Joel JJ • 25th June 2026

Simba dhidi ya Singida BS kupigwa dimba la Isamuhyo

Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba SC dhidi yaSingida BS utapigwa katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, uliopo jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa raundi ya 29 umepangwa kuchezwa Jumamosi saa 10 jioni, kama ilivyo kwa michezo mingine yote ya raundi hiyo ambayo pia itaanza kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, michezo yote ya raundi ya 29 itachezwa saa 10 jioni, huku timu zote zikipaswa kucheza mechi zao za raundi ya 29.

Uwanja wa KMC Complex utatumika kwa mchezo kati ya Yanga SC na TRA United, hali iliyosababisha Simba SC kurejea tena kucheza katika uwanja wa Isamuhyo kwa sababu JKT Tanzania watakuwa ugenini mkoani Mwanza dhidi ya Pamba Jiji.

Simba na Singida BS ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wake katika hatua za mwisho za msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ni mchezo ambao Simba inahitaji ushindi ili kuendelea kusalia kwenye mbio za ubingwa kwani kama watakosa ushindi na Yanga kushinda mchezo dhidi ya TRA United, ni wazi ubingwa utaelekea Jangwani mapema kwa msimu wa tano mfululizo

More Stories

Bayern yakamilisha usajiri wa kinda hatari
Bayern yakamilisha usajiri wa kinda hatari
Today, READ MORE →
Simba dhidi ya Singida BS kupigwa dimba la Isamuhyo
Simba dhidi ya Singida BS kupigwa dimba la Isamuhyo
Today, READ MORE →
Bingwa atajulikana Juni 27 au hadi mwisho wa msimu?
Bingwa atajulikana Juni 27 au hadi mwisho wa msimu?
Today, READ MORE →
Nne bora ya mashindano ya CAF 2026/27 imekamilika
Nne bora ya mashindano ya CAF 2026/27 imekamilika
Today, READ MORE →
Cr 7, Thierry Henry, Ibrahimovic Waingia kwenye Mjadala mzito wa Soka Mtandaoni
Cr 7, Thierry Henry, Ibrahimovic Waingia kwenye Mjadala mzito wa Soka Mtandaoni
Today, READ MORE →
Hadithi ya Kushangaza ya Eric Roy na Brest
Hadithi ya Kushangaza ya Eric Roy na Brest
Today, READ MORE →
Msigwa; Mashindano Mengi ni Ufunguo Wa Kuinua Vipaji Vya Soka
Msigwa; Mashindano Mengi ni Ufunguo Wa Kuinua Vipaji Vya Soka
Today, READ MORE →
Martin Dúbravka kutua Tottenham Hotspurs, Vicario aweka nia ya kuondoka.
Martin Dúbravka kutua Tottenham Hotspurs, Vicario aweka nia ya kuondoka.
Today, READ MORE →
Yanga yatuma ofa Al Ittihad, kumrejesha Aziz Ki
Yanga yatuma ofa Al Ittihad, kumrejesha Aziz Ki
Today, READ MORE →
Ally Kamwe, Tupo pamoja na Azam
Ally Kamwe, Tupo pamoja na Azam
Today, READ MORE →