Kenya imezidi kuonyesha kasi ya maandalizi yao kuelekea michuano ya #AFCON2027, huku ujenzi wa miundombinu muhimu ukiendelea. Mashabiki wa soka kutoka kila kona ya bara wanazidi kupata matumaini kwamba AFCON 2027 itakuwa ya kipekee zaidi kuwahi kutokea.
Uwanja huu mpya unatarajiwa kuwa kitovu cha burudani, mshikamano, na historia mpya ya soka barani Afrika. Dimba la Talanta Sports City unaendelea kuchukua sura, ishara kuwa nchi hiyo ipo kwenye hatua nzuri za kujiandaa kuwapokea mataifa na mashabiki kutoka kote Afrika.
Ikiwa imebaki takribani siku 360 kabla ya mashindano hayo kuanza, Kenya imeweka wazi kuwa ipo tayari kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika katika mazingira ya viwango vya kimataifa, huku maandalizi yakizidi kushika kasi siku hadi siku, huku uwanja huo wa kisasa ukitarajiwa kuwa miongoni mwa vivutio vikuu vya AFCON 2027. Serikali na wadau wa soka wanaamini nchi iko kwenye njia sahihi ya kuandaa mashindano yenye viwango vya kimataifa.



