Aucho kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba na Singida BS

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th June 2026

Aucho kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba na Singida BS

Kiungo mkabaji na nahodha wa timu ya taifa ya Uganda, Khalid Aucho, anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Singida Black Stars kuhusu kusitisha mkataba wake, licha ya mkataba huo kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2026/27.

Taarifa kutoka chanzo cha uhakika imebainisha kuwa pande zote mbili zimeanza majadiliano ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba huo kwa maridhiano.

Aucho alijiunga na Singida Black Stars msimu uliopita akitokea Yanga SC, baada ya kumaliza kipindi cha mafanikio cha misimu mitatu akiwa Jangwani. Hata hivyo, maisha yake ndani ya Singida BS hayajawa rahisi.

Kiungo huyo amekumbwa na majeraha ya mara kwa mara yaliyomfanya kukosa mechi nyingi za timu yake. Mbali na changamoto za majeraha, aliwahi pia kusimamishwa na klabu kutokana na tuhuma za utovu wa nidhamu kabla ya kurejeshwa kikosini.

Katika kipindi chake akiwa Yanga, Aucho alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu waliochangia mafanikio makubwa ya klabu hiyo katika mashindano ya ndani na kimataifa, kiwango kilichomfanya kuwa miongoni mwa viungo bora katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Tetesi zimedokeza kuwa Aucho huenda akarejea klabu yake ya zamani Gor Mahia ya Kenya

More Stories

Lumumba kivutio Kombe la Dunia licha ya matokeo mabaya ya DR Congo
Lumumba kivutio Kombe la Dunia licha ya matokeo mabaya ya DR Congo
Today, READ MORE β†’
Aucho kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba na Singida BS
Aucho kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba na Singida BS
Today, READ MORE β†’
Valverde na wenzake wamgeukia Bielsa, Mvutano Wazidi kambi ya Uruguay.
Valverde na wenzake wamgeukia Bielsa, Mvutano Wazidi kambi ya Uruguay.
Today, READ MORE β†’
Mtazamo wako ni upi juu ya tukio ili ?
Mtazamo wako ni upi juu ya tukio ili ?
Today, READ MORE β†’
Singida , Tukishindwa kuifunga simba hatustahili kimataifa
Singida , Tukishindwa kuifunga simba hatustahili kimataifa
Today, READ MORE β†’
Barker , Tukitumia nafasi Singida hawachomoki
Barker , Tukitumia nafasi Singida hawachomoki
Today, READ MORE β†’
Kenya wapo moto kusubiri ujio wa AFCON 2027
Kenya wapo moto kusubiri ujio wa AFCON 2027
Today, READ MORE β†’
Yanga vs TRA United, uchambuzi
Yanga vs TRA United, uchambuzi
Today, READ MORE β†’
Tunataka Ushindi TU , Moalin
Tunataka Ushindi TU , Moalin
Today, READ MORE β†’
Rais Wydad AC, Said Naciri afungwa miaka 10 jela
Rais Wydad AC, Said Naciri afungwa miaka 10 jela
Today, READ MORE β†’