Yanga, Simba zachuana kwenye ubingwa hadi mwisho

Joel JJ By Joel JJ β€’ 27th June 2026

Yanga, Simba zachuana kwenye ubingwa hadi mwisho

Mechi za ligi kuu ya NBC raundi ya 29 zimehitimishwa leo kwa vigogo wa soka nchini Ynga na Simba kuendelea kuchuana kwenye mbio za ubingwa baada zote kushinda.

Ikicheza uwanja wa KMC Complex, Yanga ikiwaadhibu TRA United mabao 3-0 kiungo mshambuliaji Allan Okello akifunga hat-trik ya nne msimu huu.

Ushindi huo umeifanya Yanga ifikishe alama 72 na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya wapinzani wao Simba.

Simba ilikuwa uwanja wa Isamuhyo ikichuana na Singida BS katika mchezo ambao Wekundu wa Msimbazi waliendeleza ubabe kwa ushindi wa mabao 2-0.

Elie Mpanzu na Anicet Oura walifunga mabao hayo na kuwahakikishia Wekundu wa Msimbazi alama tatu muhimu zilizowafanya wafikishe alama 70.

Azam Fc nayo ilikuwa mkoani Tanga kuikabili Coastal Union wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani.

Feisal Salum alifunga bao lake la 15 katika mchezo huo na kuendelea kuongoza mbio za ufungaji bora mbele ya Okello na Mossi Ndumumwe wenye mabao 14 kila mmoja.

Chini ya msimamo kuna mabadiliko yametokea baada ya Tanzania Prisons kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na kuondoka eneo la hatari kushuka daraja moja kwa moja wakiishusha Mtibwa Sugar ambayo sasa inachungulia kaburi.

More Stories

Yanga, Simba zachuana kwenye ubingwa hadi mwisho
Yanga, Simba zachuana kwenye ubingwa hadi mwisho
Today, READ MORE β†’
Misri yatinga hatua ya 32 Bora baada ya sare dhidi ya Iran
Misri yatinga hatua ya 32 Bora baada ya sare dhidi ya Iran
Today, READ MORE β†’
Kante afanana na Che Malone? makosa madogo yanayoweza kumgharimu Simba
Kante afanana na Che Malone? makosa madogo yanayoweza kumgharimu Simba
Today, READ MORE β†’
Cape Verde Gumzo la Dunia, Kutoka kuwa wageni hadi 32 bora WC2026
Cape Verde Gumzo la Dunia, Kutoka kuwa wageni hadi 32 bora WC2026
Today, READ MORE β†’
France yatinga 32 Bora kombe la dunia kibabe ikiichapa Norway, Dembele akiweka rekodi
France yatinga 32 Bora kombe la dunia kibabe ikiichapa Norway, Dembele akiweka rekodi
Today, READ MORE β†’
Senegal waandika historia kombe la Dunia, huku wakiishikilia hatma yao mkononi
Senegal waandika historia kombe la Dunia, huku wakiishikilia hatma yao mkononi
Today, READ MORE β†’
Pigo kubwa kwa England, Reece James nje kwa angalau wiki Mbili
Pigo kubwa kwa England, Reece James nje kwa angalau wiki Mbili
Today, READ MORE β†’
Lumumba kivutio Kombe la Dunia licha ya matokeo mabaya ya DR Congo
Lumumba kivutio Kombe la Dunia licha ya matokeo mabaya ya DR Congo
Yesterday, READ MORE β†’
Aucho kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba na Singida BS
Aucho kwenye mazungumzo ya kusitisha mkataba na Singida BS
Yesterday, READ MORE β†’
Valverde na wenzake wamgeukia Bielsa, Mvutano Wazidi kambi ya Uruguay.
Valverde na wenzake wamgeukia Bielsa, Mvutano Wazidi kambi ya Uruguay.
Yesterday, READ MORE β†’