Dakika 90 za mwisho za NBC Premier League zimebeba vita nyingine nje ya uwanja, vita ya benchi la ufundi kati ya Kocha Mkuu wa Yanga, Abdi Hamid Moallin, na Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker.
Wote wawili wameonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza timu zao msimu huu, lakini kila mmoja ametumia falsafa tofauti kuifikisha timu yake kwenye mbio za ubingwa hadi mchezo wa mwisho.





