Moalin - Tunahitaji Ushindi Tuwe Mabingwa

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said β€’ 29th June 2026

Moalin - Tunahitaji Ushindi Tuwe Mabingwa

Kocha wa Young Africans SC, Abdihamid Moalin, ameweka wazi msimamo wa kikosi chake kuelekea mchezo wa NBC Premier League dhidi ya JKT Tanzania, akisisitiza kuwa Yanga haiingii uwanjani kwa lengo lingine lolote zaidi ya ushindi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Moalin alisema maandalizi ya kikosi chake yamekamilika na wachezaji wako tayari kwa pambano hilo muhimu.

"Tunaingia kila mchezo kwa lengo la kushinda,"alisema Moalin kwa kujiamini, akionyesha dhamira ya mabingwa hao watetezi kuendelea na kasi yao bila kujali ukubwa wa mpinzani.

Kwa upande wake, kiungo Emmanuel Mwanengo alisema kikosi cha Yanga kinaelewa uzito wa mchezo huo, akibainisha kuwa ushindi wa aina yoyote utatosha kuipa timu hiyo ubingwa wa Ligi Kuu mbele ya mashabiki wao.

"Tunafahamu umuhimu wa mchezo huu na tumejiandaa vizuri. Lengo letu ni kushinda na kutwaa ubingwa,"alisema Mwanengo.

Kauli hizo zinakuja huku JKT Tanzania ikiwa tayari imeanza vita ya kisaikolojia kupitia mitandao ya kijamii kwa kuchapisha ujumbe wa "Last Dance", ikiashiria dhamira yao ya kuzuia Yanga kutwaa taji.

Hata hivyo, Yanga wamechagua kujibu kwa utulivu na kuonyesha imani yao kupitia maandalizi na kauli za viongozi wa kikosi, badala ya kuingia kwenye vita ya maneno.

Sasa macho yote yataelekezwa Uwanja wa Maj Gen Isamuhyo kesho saa 10:00 jioni, ambapo JKT Tanzania watakuwa wakisaka kuharibu sherehe za ubingwa, huku Yanga wakihitaji ushindi mmoja pekee kuandika historia nyingine. Dakika 90 za mchezo huo ndizo zitakazotoa jibu la mwisho.

More Stories

Moalin - Tunahitaji Ushindi Tuwe Mabingwa
Moalin - Tunahitaji Ushindi Tuwe Mabingwa
Today, READ MORE β†’
Mechi tatu kupigwa leo ndani ya kombe la dunia 2026, Hatua ya 32 Bora.
Mechi tatu kupigwa leo ndani ya kombe la dunia 2026, Hatua ya 32 Bora.
Today, READ MORE β†’
Moallin au Steve Barker, dakika 90 za mwisho za kuandika historia ya ubingwa
Moallin au Steve Barker, dakika 90 za mwisho za kuandika historia ya ubingwa
Today, READ MORE β†’
Chelsea waendelea kumuwinda Granit Xhaka, Kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao
Chelsea waendelea kumuwinda Granit Xhaka, Kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu ujao
Today, READ MORE β†’
Pamba Jiji Yakabiliwa Na Hatari Ya Kuporomoka Kikosi, Nyota Wake Wahusishwa Na Timu Mbalimbali
Pamba Jiji Yakabiliwa Na Hatari Ya Kuporomoka Kikosi, Nyota Wake Wahusishwa Na Timu Mbalimbali
Today, READ MORE β†’
JKT Tanzania : Tunatafuna mfupa uliowashinda
JKT Tanzania : Tunatafuna mfupa uliowashinda
Today, READ MORE β†’
Kinda Afrika kusini Aiteka WC2026, Atabiliwa Makubwa
Kinda Afrika kusini Aiteka WC2026, Atabiliwa Makubwa
Today, READ MORE β†’
Hatma ya Fountain Gate, Mbeya City, Mtibwa na Tanzania Prison Kufahamika kesho
Hatma ya Fountain Gate, Mbeya City, Mtibwa na Tanzania Prison Kufahamika kesho
Today, READ MORE β†’
Canada waiondoa Bafana bafana dakika za jioni, Watinga 16 bora kwa mara ya kwanza
Canada waiondoa Bafana bafana dakika za jioni, Watinga 16 bora kwa mara ya kwanza
Today, READ MORE β†’
Afrika Kusini na Canada kufungua 32 bora leo
Afrika Kusini na Canada kufungua 32 bora leo
Today, READ MORE β†’