Norway imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Côte d’Ivoire katika mchezo wa kusisimua wa hatua ya 32 Bora. Mabao ya Norway yalifungwa na Antonio Nusa dakika ya 39 na mshambuliaji hatari Erling Haaland dakika ya 86, huku Amad Diallo akiifungia Côte d’Ivoire bao pekee dakika ya 74.





